Wednesday, 14 October 2020

MASLAHI YA TAIFA HAYABEZWI ZAIDI YA KULINDWA

.William Peter Ndilla

Sumve, Mwanza.

+255759929244

October 14,2020.


Mtu Yoyote anayebeza Maendeleo Yetu Kama Taifa Maana Yake anabeza Maslahi ya Taifa la Tanzania.Mtu anayebeza Miradi Mikubwa ya Kimkakati na Kusema haya ni Maendeleo ya Vitu huyo anabeza Maslahi ya Watanzania Wote"Public Interests"


Maslahi ya Taifa"National Interest" hubebwa na dhana Kuu Kubwa tatu ambazo ni Uzalendo,Nidhamu Uadilifu.


MASLAHI YA TAIFA NI NINI?


Kwa tafsiri rahisi kabisa Maslahi ya Taifa ni Mambo Yote ambayo yanalinda Mustakabali wa Taifa fulani Kiuchumi,Kisiasa na Kiutamaduni.


Maslahi ya Taifa hujengwa Katika Msingi wa "Maslahi ya Wengi" Yalindwe na Maslahi ya Wachache Yafate.


Maslahi ya Taifa pia hujengwa Katika Msingi wa Maendeleo ya Wengi Yaanze Kuliko Maslahi ya Wachache.


MASLAHI YA TAIFA NI YAPI!


Maslahi ya Taifa hujengwa Kwenye  Kulinda na Kutumia  Rasilimali za Taifa kwa Maslahi ya Wengi"Public Interests".


Mwisho wa Siku Maslahi ya Taifa Uambatana na Kulinda Uhuru"State Sovegnity" na Umoja wa Taifa"National Unity".


Lakini pia Maslahi ya Taifa Ujengwa Katika Uwezo wa Taifa Kutafuta Maslahi yake Nje ya Mipaka kupitia Mikataba ya Kimataifa"Treaties",Biashara ya Kimataifa Wakati Mwingine Kushiriki Shughuli za Kiulinzi na Usalama Nje ya Nchi.


Kwa Mfano,hili Kulinda Maslahi ya Nchi,Tanzania italazimika Kulinda amani ya Nchi za  Maziwa Makuu ili Kuhakikisha haileti hadhari za Kivita.


Uwepo wa Wakimbizi wa Burundi Katika Tanzania kwa Miaka Zaidi ya Kumi Ungeweza Kuhatarisha Maslahi ya Tanzania Kiusalama Kuliko Kama ambavyo Burundi Ingekuwa na amani.


MASLAHI YA TAIFA MLINZI WAKE NI NANI?


Mlinzi Namba Moja wa Maslahi ya Taifa ni Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Nchi ya Tanzania. Mtu Huyu Uapishwa Kuyalinda na Kuyatetea Maslahi hayo ya Taifa dhidi ya Adui wa Ndani au Adui wa Nje.


Hili Rais aweze Kuyalinda Maslahi hayo ni lazima Rais huyu awe na tabia za Kipekee Tatu Kubwa.


Moja,MZALENDO,Mzalendo ni Mtu ambaye Yupo tayari kufa kwa ajili ya Kulinda Maslahi ya Taifa lake"Uhuru,Uadilifu,nidhamu,heshima,Umoja,Maadili na tunu za Taifa bila aibu Yoyote.


Mbili,MUADILIFU,Madilifu ni Mtu ambaye anayashinda Maslahi yake binafsi,ya Ndugu Zake au Jamaa zake kwa ajili ya Kulinda Kwanza Maslahi ya Wengi"Public Interests".


Watu hawa huweza kuzishinda tamaa Zao Kifedha,Kimadaraka,na Kimwili pia kwa ajili ya Manufaa ya Wengi au ili Kuweza Kulinda haki za Wengi.


Tatu, NIDHAMU,Nidhamu pia ni Sehemu ya Sifa Kuu ya Rais Mzalendo. Nidhamu ni hali ya Kusimamia Mambo Mliyokubaliana Kwa Kuzingatia Mda na Ubora wa huduma Unayotoa Kwa Watu.


Rais anapaswa Kulinda Kiapo Chake Cha Kikatiba Cha Kulinda Maslahi ya Taifa bila Kuyaonea aibu dhidi ya Wanaotafuta Kuyabomoa Maslahi hayo.


WANANCHI au Raia ni Kundi la Pili Katika Kulinda Maslahi ya Taifa kwa Kuhakikisha Wanafanya Kazi Hili Kupiga hatua za Maendeleo Katika Nyanja Zote za Maendeleo.


MASLAHI YETU KAMA TAIFA NI YAPI?


Amani Yetu Kama Taifa ndio Maslahi Yetu,Uhuru Wetu Kama Taifa ndio Maslahi Yetu,Rasilimali Zetu Kama Taifa ndio Maslahi Yetu,Umoja Wetu Wetu ndio Maslahi Yetu Kama Taifa,Tunu Zetu Kama Taifa ndio Maslahi Yetu,Miradi Yetu Kama Taifa ndio Maslahi Yetu na Kwa Ujumla Maendeleo Yetu Kama Taifa ndio Maslahi Yetu."Common Interests".


KUMDHARAU RAIS NA AMIRI JESHI WETU NI KUTUKANA MASLAHI YETU KAMA TAIFA.


Tunasema Rais ndio Mlinzi Namba Moja wa Maslahi ya Nchi,Rais Utumia Vyombo Vyake vya Dola Kulinda Maslahi hayo.


Kwahiyo Kumsema Vyovyote Rais Kwa lengo la Kumvunjia heshima Mfano Juzi Mh. Tundu Lissu Mgombea Urais Kwa tiketi ya Chadema akiwa Kwenye Mkutano Wake wa Kampeni alisikika akisema.."......Rais Magufuli anafikiri Sisi ni Washamba Kama Yeye.....Benki gani Utapata Mkopo Kwa Kitambulisho kile....hakina Picha,hakina Jina.......".


Kiufupi Tundu Lissu anahatarisha Maslahi ya Taifa na Asije akashangaa Walinda Maslahi hayo "Wakimrukia".


Rais Bora wa awamu ya tano lazima aweze kuyajua na Kuyalinda Maslahi ya Taifa lake.


KURA Yako Kampeni Mgombea anayelinda Maslahi hayo Kwa ajili ya Vizazi Vya leo na Kesho,Rais John Pombe Magufuli anakuhakikishia Ulinzi wa Maslahi hayo.


Chagua John Pombe MAGUFULI,Chagua Chama Cha Mapinduzi, Chagua Maendeleo.

No comments:

Post a Comment