NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Jumla ya makarani waongozaji 960 wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 28, jimbo la Arusha mjini wamepewa mafunzo na kuapishwa tayari kwa zoezi la uchaguzi.


Akizungumza na waandishi wa habari  mkurugenzi wa jiji la Arusha Dr John Pima alisema kuwa mafunzo hayo yataendelea kwa siku tatu ambapo pia yatenda sambamba mafunzo ya wasimamizi namba moja wa vituo vya wapiga kura pamoja na wasimamizi namba mbili


“Hatua hii ni baada ya kumaliza zoezi la kuwaapisha mawakala wa vyama vya siasa kutoka vyama 15 vinavyoshiriki uchaguzi mkuu katika jimbo hili” Alieleza Dr Pima.


Aidha alifafanua  kuhusiana na kiapo cha mawakala kuwa wapo katika hatua ya kuzichakata na kuzirudisha kwa vyama vya siasa nakala zao.


Dr Pima pia alitumia fursa hiyo kuwasisitiza na kuwaomba wananchi wa jiji la Arusha siku ya uchaguzi wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kutumia viruzi haki yao kumchagua viongozi wanayemtaka.


“Arusha yetu bado ina amani na utulivu na shughuli zote zinaenda vizuri na hata siku ya uchaguzi ambayo ni siku chache kutoka leo tunaamini itakuwa nzuri” Alisisitiza.


Alifafanua kuwa uchaguzi katika jiji la Arusha utakuwa huru na haki hivyo wananchi wasiwe na hofu na waachane na maneno na mambo yanayosemwa kwani hayo ni mambo ya wanasiasa na sio kweli.


“Yapuuzieni hayo yanayosemwa kwani wanasiasa mara nyingine wanafika kipindi wanakuwa na mambo yao lakini sisi kama tume tunasema kuwa kila kitu kiko vizuri hivyo tulieni na mpuuze yanayosemwa kwani hayana maana yoyote” Alifafanua.


Sambamba na hayo pia aliwataka viongozi wa dini na mila kuendelea kuwahimiza watu kujitokeza kwenda kupiga kura kwasababu hali itakuwa salama na hakutakuwana shida yoyote.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: