NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Laban Kihongosi ameongoza matembezi ya kumuenzi baba wa taifa hayati mwalimu Julias Kambarage Nyerere lengo likiwa ni kuhamasisha kuendeleza na kulinda tunu ya amani aliyo tuachia.


Akizungumza katika matembezi hayo yaliyohitimishwa katika mnara wa azimio la Arusha(Mnara wa Mwenye) Kenan alisema kuwa hayati Mwalimu Nyerere amefanya mambo mengi ikiwemo kuleta uhuru uliowafanya watanzania kuwa na amani hivyo kila mwananchi atambue kuwa ana wajibu wa kuilinda na kuendeleza amani.


Alieleza kuwa katika kumuenzi baba wa taifa wilaya ya Arusha wameona wafanye matembezi ya kumuenzi ili kuwaeleza watanzania kwamba wana wajibu wa kuendeleza amani iliyoasisiwa na viongozi ambao bila wao na jitihada zao  vijana, akina mama, kina baba na wazee wasingeweza kufaidi matunda hayo ya amani.


“ Pia kupitia matembezi haya  nafikisha ujumbe kwamba kuelekea uchaguzi mkuu tunapenda tuende tukatunze na kulinda amani yetu” Alisema Dc Kenan.


Pia alifafanua kuwa wamehitimishia matembezi hayo katika mnara wa azimio la Arusha kutokana na umuhimu wa eneo hilo ambapo mwaka February 5,1967 azimio hilo lilianzishwa na waasisi ambapo pia eneo hilo limewekwa mnara mwenge ambao una maana kubwa kwa watanzania.


“Jukumu au kazi kubwa ya mwenge ni kumulika mipaka ya nchi yetu nani na nje, kuleta matumaini mahali ambapo hakuna matumaini, upendo palipo jaa chuki lakini pia kusababisha mambo mazuri ya maendeleo ya nchi yetu” Alisema.


Aidha  alisema watanzania hasa vijana wanawajibu wa kujua historia ya nchi yao kuweza kuienzi na  kuirisha vizazi na vizazi pamoja na kujua nchi imetoka wapi, iko wapi na inaenda wapi ambapo bila kujua hayo wataishia kulalamika tu.


Kwa upande wa baadhi ya wananchi Kibuzo Senga Kibuzo alisema watanzania wanapaswa kumenzi Mwalimu hasa kwa kufanya kazi kwaajili ya maendeleo yao ambapo alisema uhuru na kazi 


“Mtu yoyote maendeleo yake yanatokana na juhudi zake na hakika tunakumbuka  mazuri na mengi ya baba wa taifa alijitoa muanga kwajili ya watanzania huo ulikuwa ushindi mkubwa ndo mana leo tunajivunia,” Alieleza Kibuzo.


Naye Esther Kivuyo Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Felex Mrema alisema kuwa anamfahamu mwalimu Julias Nyerere kama baba wa taifa aliyeleta uhuru na maendeleo na matembezi hayo yanaonyesha ni jinsi gani watu wa Arusha walivyonufaika na uongozi wake.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: