Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka, akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akitangaza kuwa chuo hicho kinatarajia kuanza ujenzi wa tawi lake jijini Dodoma.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka, akisisitiza jambo kwa na waandishi wa habari leo wakati akitangaza kuwa chuo hicho kinatarajia kuanza ujenzi wa tawi jipya jijini Dodoma kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Benny Mwaipaja.

Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka,(hayupo pichani)wakati akitangaza kuanza kwa ujenzi wa tawi jipya la chuo hicho jijini Dodoma.

Maafisa kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha wakifatilia Mkutano huo.

Mipango Benny Mwaipaja,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma wakati Chuo cha Uhasibu Arusha kinatangaza kuanza ujenzi mpya wa tawi lake.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa chuo hicho mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa chuo hicho jijini Dodoma.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao kuhusu ujenzi wa chuo hicho jijini Dodoma

......................................................................................................
Na Alex Sonna ,Dodoma
CHUO cha Uhasibu Arusha(IAA), kinatarajia kufungua tawi lake Jijini Dodoma Desemba mwaka huu kwa ajili ya masomo ngazi ya shahada ya uzamivu na mafunzo ya muda mfupi kwa mawakala wa benki na wanaoendesha huduma za fedha kwa njia ya simu.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Mkuu wa Chuo hicho, Prof.Eliamani Sedoyeka, amesema kitaanza kutoa masomo hayo kwenye jengo la kupanga huku wakitarajia kuanza ujenzi wa majengo yao Januari 2021 kwenye eneo la Njedengwa.
Amesema kuwa hatua hiyo inatokana na nusu ya wanafunzi wa shahada ya uzamivu kuwepo Dodoma, hivyo Chuo kinafungua tawi hilo ili kurahisisha utoaji elimu na kuunga mkono jitihada za serikali kuhamia Dodoma.
Prof.Sedoyeka amesema watajenga kwa kutumia utaratibu wa ‘force account’ ili kuanza kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya astashahada.
Kuhusu mafunzo ya muda mfupi, Mkuu huyo amesema yatatolewa kwa wiki sita na yanalenga kuchochea masuala ya kiuchumi ili kuwepo na uchumi shirikishi wenye weledi na ujuzi.
Amebainisha kuwa katika Mpango Mkuu wa Maendeleo Sekta ya Fedha nchini wa miaka 10, Taasisi za elimu ya juu nchini na taasisi za utafiti zimeagizwa kutumia fursa zilizo kwenye mpango huo ili kujipanga katika kuboresha maeneo ya kitaalamu na kiutafiti ili sekta iendelee kukua na kuhimilia ushindani na mabadiliko.
“Kwenye Mpango kuna maagizo kwenye taasisi za elimu ili kufanikisha kufikia malengo hayo, tukaamua kuanzisha course za muda mfupi ambazo zitakuwa za wiki sita kwa Agent Banking na Mobile money kutokana na sekta hii ndio inaonekana kukua kwa kasi lakini watoa huduma hawana utaalam huo,”amesema.
Amesema sekta hiyo inakua kutokana na uwekezaji wa serikali kwenye masuala ya mawasiliano na upatikanaji wa umeme ambapo huduma hizo zipo hadi maeneo ya vijijini hivyo mafunzo hayo yatakuwa ya muhimu kwao kuwa wabobezi kwenye utoaji wa huduma hiyo.
“Ili kuendana na jitihada za serikali tumejipanga kutoa mafunzo haya ambayo yatawafikia moja kwa moja watanzania, hii sekta ndogo ya fedha sio ndogo kama tunavyofikiri ndio eneo ambalo watanzania wengi kwasasa wanatumia, tunaamini hatua hii itasaidia kutambua biashara hiyo lakini pia kujua namna ya kuiendesha,”amesema.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo kwasasa yatatolewa Arusha, Dar es salaam na Dodoma na baadaye yataenda kwenye maeneo mengine.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: