Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi tamasha la "Karibu Dodoma "linalotarajiwa kufanyika Oktoba 22-24 Jijini hapa.

Lengo la tamasha hilo ni kupongeza juhudi za Rais John Magufuli katika kukuza na kutangaza mkoa na Jiji la Dodoma ikiwa ni sehemu za kuendeleza fikra za baba wa Taifa juu ya makao makuu kuhamia Dodoma.


Hayo yamesemwa leo  Jijini Dodoma  na Mratibu wa tamasha hilo Saimon Mwapagata (Rado)wakati akizungumza  na waandishi wa habari .

Mwapagata amesema tamasha hilo 'karibu Dodoma Festival'litakuwa na maudhui ya Kutoa fursa kwa makundi mbalimbali ya jamii na kwenye sekta mbalimbali ambazo zimefanya vizuri na kuleta mabadiliko  chanya kwa jamii.

"Tunatumia Jiji la Dodoma katika kuratibu mambo makubwa yanayo unganisha Taifa kwa sababu Dodoma ndio makao makuu ya nchi ,"amesema.

Licha ya hayo amebainisha kuwa kuwa katika kutoa fursa ilivyokusudiwa makundi ya jamii pamoja na sekta mbalimbali zitapewa nafasi ya Kutoa ushihuda wa mabadiliko yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa  Dk.Jonh Magufuli.


"Tunapaswa kutoa shukrani zetu kwa Serikali ya awamu ya tano,na katika kufanya hivyo Kuna baadhi ya makundi yaliyopata mabadiliko ya ushindi ndani ya miaka makundi hayo yatapata nafasi ya kueleza ushindi huo;

Makundi hayo ni Pamoja na bodaboda,mama ntilie,machinga,watu Wenye ulemavu ,wanafunzi wa vyuo ,vijana,wanawake na Wazee"alifafanua.


Hata hivyo aliweka sawa suala hilo kwa kusema kuwa halipo kisiasa na kwamba Wananchi wanapaswa kutofautisha tamasha hilo na nguvu ya siasa .

Kwa upande wake Katibu wa jumuiya ya watu wenye ulemavu Tanzania John Mlabu alisema ,kundi hilo linatambua mchango wa Serikali ya awamu ya tano hivyo kwa nguvu moja wameamua kuunga mkono tamasha hilo.

"Tuneshuhudia Rais akiwajali walemavu kwa vitendo ,jamii ilizoea kuona walemavu wakiwa ombaomba ,maisha yao yalikuwa magumu,lakini Sasa hali imebadilika tuna nafasi ya kufanya biashara na kujijenga kiuchumi,"amesema.

Naye mwakilishi wa wanawake wajasiriamali Jijini Dodoma  Mariam Fentu alieleza kuwa ni Wakati wa kuyaweka hadharani mambo waliyifanyiwa na Serikali ya Magufuli ambapo alisema imewashika mkono kwa asilimia 99.

"Tukimkopesha Magufuli kura zetu na Sasa anatulipa maendeleo kwa vitendo,tunafanya biashara kwa mikopo nafuu ya asilimia 4 iliyotolewa na Serikali kwa kundi la wanawake"amesema..



Mwisho.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: