Na  Woinde Shizza Michuzi TV

Shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Rukwa limeendelea kufanya uhamasishaji na utoaji elimu kwa Wananchi wengi wa Vijiji vilivyopitiwa  na mradi wa usambazaji umeme vijijini-wa REA wananchi wengi wamehamasika sana juu ya huduma za umeme wakati wa kampeni hiyo ya Uhamasishaji na utoaji elimu mbalimbali za huduma ya umeme.

Kampeni hiyo imeendeshwa na mwakilishi kutoka Idara ya masoko ya shirika la umeme TANESCO  Sylivesta Matiku akishirikiana na Afisa Uhusiano Saidy Mremi.

Uhamasishaji huo uliwezesha vijiji zaidi ya 25 vilivyoko wilaya za Sumbawanga Laela, Kalambo na Nkasi kupata elimu mbalimbali zinazohusu huduma za umeme.

Uhamasishaji huo wa utoaji elimu uliwezesha wananchi  kujua taratibu za Kuunganisha umeme, elimu ya usalama, ulinzi wa miundo mbinu,  tahadhari ya ajali za umeme, elimu ya matumizi bora ya umeme na jinsi ya kujiepusha na matepeli (vishoka).

Miongoni mwa Vijiji vilivyonufaika na elimu hizo ni Kaengesa, Lyapona, Mpombwe, kapozwa,¹ kalambo,kilewani, kalemashi, katili kipanga, vingine vitakavyonufaika ni kazovu, korongwe, kabwe, mbende, katani, Zimba, Nankanga, kizumbi, mpui, miangalua,Lowe, kalambezi, Tunko,Kianda, Lowe.

Mradi wa umeme wa REA wa  awamu ya tatu mzunguko wa kwanza unaotekelewa na na mkandarasi wa NAKUROI umewezesha vijiji 120 kupata ya huduma yah umeme.

Mradi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90% wananchi wanaokadiriwa kuunganishwa ni wateja zaidi ya 3500  kwa njia moja na umeme wa njia tatu

162 picha ikionyesha mwakilishi kutoka Idara ya masoko ya shirika la umeme TANESCO  Sylivesta Matiku akitoa elimu kwa wananchi wa Sumbawanga

175 picha ikionyesha Afisa Uhusiano  wa TANESCO Saidy Mremi akiendelea kutoa elimu kwa wananchi wa Sumbawanga laela
Share To:

msumbanews

Post A Comment: