Saturday, 19 September 2020

UAMINIFU,UTII NA KUJITOA KUNALIPA NDANI YA CCM YA JOHN MAGUFULI


William Peter Ndilla.
Sumve,Mwanza.

Maisha ya Siasa Utawaliwa na Mambo Mengi kiasi kwamba yanahitaji Ukomavu wa hali ya Juu. Watu wenye Kariba za Aina ya *Dkt Mwigulu Lameck Nchemba* Wana nafasi Kubwa ya Kukua na kuaminika kwa Jamii na Kwa Wakuu kwa Sababu ya tabia Zao.

Maisha ya Siasa ni Kama maisha ya Mpira wa Miguu,ni maisha ya Kutoka na kuingia kwenye "System" na Ni Mwanasiasa Mjinga tu ambaye atachukia baada ya kukosa Uteuzi au nafasi ya kuwatumikia Watu.

Kwa bahati Nzuri Wanasiasa Wengi wa  Tanzania Walikuwa hawalijui hili kwa muda mrefu maana Wengi baada ya kukosa Uteuzi walipayuka na kuhangaika Sana" Kuna mifano ya wengi na wakarudi wakiomba radhi na kusamehewa ingawa sasa tunajifunza mapema ili tusije omba radhi tena.

Bahati Nzuri baada ya Matokea ya Uteuzi Ndani ya CCM nimeona Kuna Wanasiasa wakongwe walishiriki na wanaendelea kushiriki Katika Shughuli za CCM hasa hizi za Kuwaombea Kura wateule wa CCM Katika nafasi za Ubunge na Udiwani.

Hii Ndio sifa ya Mwanasiasa mwenye Malengo Makubwa na ya Mda mrefu ni lazima ajifunze kuishi Katika Mambo Makubwa Matatu.

Moja Utulivu,Uvumilivu na Unyenyekevu Mkubwa.Hii Ndio sifa kuu ya Mwanasiasa anayetaka kwenda mbali Katika kuwatumikia Watu na lazima akumbuke kuwa Mnyenyekevu leo,Kesho na Kesho kutwa kwa Wakubwa zake wa wakati huo.

Mfano mzuri Ni *Dkt Lameck Mwigulu Nchemba* ambaye baada ya Uteuzi wake kutenguliwa aliendelea kuisemea CCM Ndani ya Bunge kwa hoja na NGUVU Kubwa.

*Lameck Nchemba* ilikuwa lazima arudishwe kwenye System Sababu alionyesha Utulivu na Unyenyekevu wa hali ya Juu.

Sifa ya Pili ni Uaminifu,Utii kwa Mamlaka na Unyumbulifu.Katika Serikali ya awamu ya tano idadi Kubwa ya Viongozi walitumbuliwa lakini Wengi pia walipewa nafasi zingine"Second Chance".

Nini kiliwapa "Second Chance?",Uaminifu kwa Mamlaka ya Uteuzi na Utii wa kukiri makosa na Kupata msamaa.Hakuna Uchawi Kama Unataka Kukua kwenye Siasa Zaidi ya Uaminifu,Utii na Unyumbulifu"Flexibility".

Tatu ni Uchapakazi na Kujitoa kwa ajili ya Chama au Serikali.

Pia hapa mfano wangu Mkubwa utakuwa *Mwigulu Nchemba* ambaye kwa hakika Katika Majukumu Yote aliyopewa akiwa Wizara ya fedha alifanya kwa Uaminifu Mkubwa na Kuendelea kutumia Ubunge wake kujibu hoja za Upande wa Pili.

Kiongozi Aina ya JPM hawezi kukuacha Kama una Kariba hizi Sababu *John Joseph Pombe Magufuli* Kila siku ni Kiongozi wa kutoa Nafasi Nyingine"Second Chance".

Faida za Kujitoa Katika Serikali na Chama Katika awamu hii ni Kubwa  na zinaonekana kutambulika.

Teuzi zote za John Pombe Magufuli Zina Sababu nyuma yake Kama Sio "record zako"basi itakuwa Uaminifu wako,Kama Sio Uaminifu wako basi ni Unyenyekevu wako na Kama Sio hivyo Vyote basi ni Utii  Wako.

Faida za Mwanasiasa kuishi Katika tabia hizi ni nyingi Sana Kama vile.

Kuaminika kwa Wakuu na Kwa Mamlaka za Wateuzi.Mwanasiasa Mwenye tabia hizi anaaminika Zaidi kuliko Asiye na tabia hizi.

Mwanasiasa wa namna Hii lazima atapewa Majukumu Mazito Katika Chama na Serikali.Uteuzi wa Albert Chalamila Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ni matokeo ya kuwa na tabia hizi na baadae akapewa Jukumu la kutafuta Mali za CCM na baaae akaishia kuapata Uteuzi Mkubwa Katika Mkoa "Giant",Mkoa wa Mbeya.

NGUZO KUU YA SIFA HIZO HAPO JUU NI UZALENDO KWA NCHI NA CHAMA NA KUWA NA HOFU YA MUNGU.

Hili kuweza kuziishi Sifa hizo kuu Tatu za hapo Juu lazima uwe na kitu kikubwa Zaidi ambayo ni HOFU YA MUNGU na UZALENDO.

Vijana wa CCM na wa Vyama Vingine Kama wanataka Kukua Kisiasa na Kuweza Kuaminika kwa Mamlaka za Uteuzi lazima Waenende Katika Njia hizi.

+255759929244.
*Bill Ndilla kama Ndilla

No comments:

Post a comment