Na John Walter-Manyara

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imeendelea kukutana na wananchi katika wilaya mbalimbali za mkoa huo kusikiliza malalamiko mbalimbali yanayohusu rushwa ili kuitokomeza.

 Mkuu wa Taasisi hiyo wilaya ya Simanjiro Wakili Adam Kilongozi  akizungumza na wanakijji wa Ngage kata ya Loborsoit amesema wamebaini kuwa Malalamiko makubwa Katika eneo hilo yanahusiana na ugawaji wa Mashamba bila kuzingatia sheria na  kanuni za ugwaji ardhi ya Kijiji.

Kilongozi amesema wengi wamelelalamika kuhusu ardhi ya kijiji kuhodhiwa na watu ambao sio wanakijiji na ugawaji wa ardhi unaolenga kuwaongezea ardhi watu ambao tayari wanazo na kuwaacha wasionazo pamoja na kugawa ardhi kwa kupendelea watu wenye uwezo kifedha.

Amesema baada ya kuzipokea kero hizo Takukuru wilaya ya Kiteto imeanzisha uchunguzi kwa lengo la kubaini ukiukwaji huo.

Mkutano huo wa hadhara ulihudhuriwa na Viongozi wa dini ya Kiislam na Kikristo ambao walipata nafasi ya kufanya Maombi kwa Mungu.


Share To:

Post A Comment: