NA ANDREW CHALE, CHALINZE

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, aliyepita bila kupingwa Mhe. Ridhiwani Kikwete amemnadi na kumuombea kura za ushindi mgombea Urais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mgombea Udiwani Kata ya Mbwewe Ndg. Omary Msonde wa Kata ya Mbwewe.

Akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni ya Udiwani Kata ya Mbwewe, Mhe. Ridhiwani Kikwete aliwaomba Wananchi kuwa na imani na Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuendelea kuwachagua kwa kura nyingi za ushindi kutokana na kazi kubwa ya Iliyofanyika miaka mitano iliyopita.

"Wananchi wa Mbwewe, Halmashauri ya Chalinze wanatarajia mazingira mazuri katika nyanja zote za maisha kuanzia kwenye Elimu , Afya, Miundombinu, Maji, Mikopo ya Wakinamama , Vijana , na walemavu." Alisisitiza Mheshimiwa Mbunge.

Akizungumzia kuhusu Elimu, Mheshimiwa Mbunge alisisitiza kuwa Wamejipanga kuhakikisha kuwa vijana wanaendelea kusoma kwenye mazingira mazuri ikiwemo ujenzi wa madarasa, Ujenzi wa nyumba za Walimu lakini pia kuhakikisha Vijana wetu wanapata elimu iliyo bora na sio bora elimu.

Sababu ni nyingi sana lakini kwa kumchagua Diwani wa Chama cha Mapinduzi na Raisi anayetokea Chama Cha Mapinduzi ndugu yetu Omary Abass kura nyingi za ushindi ni kukaribisha maendeleo kwa mbwewe mpya ya maendeleo". Alisema Ridhiwani Kikwete.

Ridhiwani Kikwete amewaomba pia Wananchi hao wa Mbwewe kumpigia kura nyingi za ushindi hiyo Oktoba 28 kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili kufanya shughuli zake kama mbunge kwenye kutatua kero zile kubwa zinazohitaji nguvu ya Mheshimiwa Raisi kuwa raisi. Kwa kumchagua mheshimiwa Raisi maana yake tumechagua kupeleka maji kwenye vitongoji, umeme vitongojini, na muhimu zaidi ni Wilaya ya Chalinze.",Alisema Ridhiwani Kikwete.

Aidha, aliwahakikishia vikundi vya Vijana, kina Mama  wananchi kwa ujumla na walemavu wakiendelea kupata mikopo isiyo na riba inayotoka Halmashauri. "Katika kipindi cha miaka 5, zaidi ya Tsh. 3 Bilioni zimewafikia makundi mbalimbali hasa makundi ya Wakina mama japo kuna baadhi ya vijiji kutokana na taratibu katika usajili wa vikundi bado havijafikiwa na fursa hii.
                 
"Natambua kwamba baadhi ya Vijiji hazikupata fedha za kutosha, lakini Mwarobaini wake anao Omary Abass ambaye mtakapomchagua Oktoba 28,  tunakwenda kufanyia kazi na kuhakikisha vikundi vyote vinaenda kusajiliwa na kupata mikopo hiyo kwa watu wote" Alisema Ridhiwani Kikwete.

Akizungumzia suala la Maji na Afya, alisema tayari changamoto hizo zimefanyiwa kazi na zilizopo bado zinaendelea kutatuliwa na watakikisha Wahudumu wa afya na vifaa tiba vinaongezeka zaidi katika awamu ya tano inayokuja.

Kwa upande wake Mgombea Udiwani wa Kata ya Mbwewe, Omary Abass amewaomba Wananchi kumpigia kura nyingi za ushindi ili awatumikie kwa moyo moja na kuleta maendeleo.         

Mwisho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: