Friday, 18 September 2020

MWENYEKITI WA TUME YA MADINI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA


Leo tarehe 18 Septemba, 2020 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ametembelea mabanda ya Wizara ya Madini na Taasisi zake kwenye Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Kituo cha Uwekezaji Bombambili Geita Mjini.

Taasisi zilizopo chini ya Wizara zinazoshiriki katika maonesho hayo ni pamoja na Tume ya Madini, Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (TEITI) Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na  Mgodi wa STAMIGOLD.

No comments:

Post a comment