Thursday, 17 September 2020

Mtega : Nina Jeshi Kubwa sana Nyuma Yangu


Na Esther Macha, Mbeya

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mbarali kupitia chama cha mapinduzi,Francis Mtega amesema ana jeshi kubwa nyuma yake ambalo linamshauri  mambo ya msingi na namna ya kuendeleza wilaya ya Mbarali .

Amesema kuwa amekuwa akipokea ushauri kila siku namna ya kuendeleza wilaya ya mbarali hivyo hata sasa naamini  kuwa nina uwezo mkubwa wa kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.

Mtega amesema hayo jana wakati  wa mkutano wa kampeni  katika Kata ya Rujewa wilayani Mbarali Mkoani Mbeya ambapo alisema ana jeshi kubwa ambalo lipo nyuma ambalo linamshauri vitu mbali mbali vya msingi ambavyo lengo ni kuiendeleza wilaya ya mbarali  na wananchi wake.

Akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Mbarali kupitia chama cha mapinduzi   Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya (CCM)Bashiru Madodi alisema wamchague Mtega ili aweze kuwaletea maendeleo wanambarali  na kwamba wachague mtu ambaye wannamuona na wanapokuwa na changamoto inakuwa rahisi kusaidiwa kuliko mtu anayetoka nje ya nchi .

Mwisho.

No comments:

Post a comment