Tuesday, 22 September 2020

MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUWA HISTORIA CHALINZE-RIDHIWANI KIKWETENA ANDREW CHALE, CHALINZE

MIGOGORO baina ya Wakulima na Wafugaji katika Halmashauri ya  Chalinze imeelezwa kuwa inaundiwa mikakati thabiti kwa kujengewa misingi imara baina ya pande zote mbili kufuatia sera nzuri ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika kuimaliza na kuwa historia.

Hayo yameelezwa na Mbunge Jimbo la Chalinze ambaye amepita bila kupingwa Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa nyakati tofauti katika mikutano yake ya ndani na ile ya wazi kwenye Kata za Jimbo hilo.

Akiwa kwenye Vijiji mbalimbali ikiwemo Vijiji Kweikonje na Mizimbani wakati wa kuwaombea kura za ushindi kwa Mgombea Udiwani wa  Kata ya Miono, Juma Mpwimbwi na Mgombea Urais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Akizungumza suala la migogoro ya ardhi baina ya Wakulima na Wafugaji inayosababisha vurugu za mara kwa mara, ni kutokana na viongozi wa Vijiji jirani kuruhusu mifugo kupita na kuja maeneo ya wakulima na kuamsha vurugu.

"Tatizo kubwa tulionalo hapa ni wenzetu wa vijiji jirani kuruhusu mifugo ipite kwenye vijiji vyao ili mabaraa yawakute watu wengine.

Kwa mfano mifugo kutoka Mvomero  wanafika pale Mpaji na kusagwa hadi kuingia huku. Tatizo hili lazima lidhibitiwe ili ng'ombe hao wasipite kwenda vijiji vingine vya mbele." Alisema Ridhiwani Kikwete.

Aidha, alisema baada ya uchaguzi kuisha watakaa na Wenyeviti wote wa Vijiji kulishughulikia jambo hilo kwa pamoja na kudhibiti.

"Ndani ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imeelekeza kuendelea kutengwa maeneo maalum kwa ajili ya wafugaji ili nao wapate maeneo ya kulisha mifugo yao na kuondoa ghasia kwa amani.

Moja ya eneo Mkoa wa Morogoro kule Mvomero limetengwa kwa ajili ya wafugaji kulisha mifugo yao... kule ilionekana ni chanzo kikubwa cha migogoro katika eneo letu hili la Kanda  ya Pwani ikiwemo Bagamoyo." Alisema Ridhiwani Kikwete.

Katika hatua hiyo, Ridhiwani Kikwete alipokea maoni mbalimbali ya Wajumbe hao kwa ajili ya kufanyiwa kazi ikiwemo suala la kuimalisja huduma za barabara, elimu, afya na masoko.

MWISHO.

No comments:

Post a comment