Wednesday, 23 September 2020

ENG. MAGANZA WA TLP AOMBA KUCHAGULIWA UBUNGE JIMBO LA KIBAMBA, AMPIGIA DEBE KURA ZA USHINDI RAIS MAGUFULINA MWANDISHI WETU.

MGOMBEA Ubunge kupitia Chama Cha Tanzania Labour Party  (TLP),
 Eng. Aivan Maganza amesema endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo atatengeneza ajira kwa wote na kutafuta wafadhil mbalimbali kwa ajili ya kusaidia vijana kupata ajira

Alisema lengo la mpango wake huo ni  kuwafanya waondokene athari za mlundikano wao mitaani baada  ya kumalizia elimu ya vyuo vikuu.

Hata hivyo mgombea huyo amesema yeye na chama chake wanamuunga mkono mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwa ndiye chaguo lao kwa upande wa Urais hivyo amemuombea kura nyingi za ushindi hiyo 28 Oktoba.

Aidha Eng.Aivan  alisema atahakikisha jimboni hapo wananchi wanapata bima z afya na kisimamia swala la wazee kupata huuduma bure.

Eng.Aivan aliongeza kuwa atasimamia Jimbo hilo kisimamia kujenga mabweni ya wanafunzi na kuweza kupata elimu bora na kujenga madaraja imara kuepusha watoto kusombwa na maji.

Eng. Aivan alimaliza kwa kusema kuwa madiwani wa chama hicho walienguliwa na tume ya Taifa ya uchaguzi hivyo wapo tayari kufanya kazi na madiwani watakaochaguliwa bila kujali vyama wanavyotoka.

Pamoja na hilo mgombea huyo pia ameahidi  kuunda mabaraza ya vijana,wanawake na wazee katika Jimbo zima bila kujali vyama ili kutoa fursa ya kuzungumzia suala la  maendeleo

Mwisho.

No comments:

Post a comment