NA HERI SHAABAN

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Bonah Ladslaus Kamoli amesema akichaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo Mikakati yake 2025 kuboresha miundombinu kuwa ya kisasa.


Bonah aliyasema hayo leo, katika mkutano wa Jimbo wakati wa kuomba kura Kata ya Kipawa Halmashauri ya manispaa ya Ilala .


"Katika uongozi wangu nitatekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi mikakati yangu 2025 kwa kushirikiana na Serikali kujenga Barabara  za kisasa Katika Mradi wa kuboresha makazi DMDP ndani ya jimbo la segerea.


Alitaja barabara hizo zitakazo pita mradi wa UMDP Kata za kipawa, Bonyokwa na Kinyerezi zote zitafikiwa na miradi ya  kuboresha miundombinu ya kisasa "alisema Bonah.

Bonah alisema   kwa kushirikiana na Serikali atakapochaguliwa baadhi ya kata hizo za Jimbo la Segerea pia zitajengwa barabara mradi wa Mabasi yaendayo haraka.
.
Aliwataka wakazi wa jimbo Segerea kumchagua ili aweze kuwa Mbunge pamoja na kumpigia kura Dkt.Rais John Magufuli na madiwani wa Segerea ili washirikiane katika kuleta maendeleo.

Bonah alisema mikakati yake mingine kuboresha sekta ya afya,Maji na Sekta ya elimu ambapo kipawa atajenga kituo cha afya kitakachotoa huduma ya mama na mtoto.

Mikakati yake mingine kutoa mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ili waweze kujiajili wenyewe wajikwamue kimaisha.

Kwa upande wake mgombea udiwani wa Kata ya Kipawa Aidan Amos alisema akichaguliwa kuwa diwani katika uongozi wake mikakati yake ya kwanza kuboresha usafi ndani ya kata hiyo ili iwe safi.

Amos alisema mikakati yake mingine kuwawezesha Wazee na Vijana na watu wenye makundi maalumu ili waweze kujishughulisha na kujikwamua kiuchumi .

Mwisho
Mkutano wa Kampeni Jimbo la Segerea kata ya Kipawa BONAH Ladslaus Kamoli
Septemba 15/2020
Share To:

msumbanews

Post A Comment: