Monday, 21 September 2020

ASIA HALAMGA AENDELEA KUTIMUA VUMBI MANYARA


Mbunge Mteule wa Viti Maalum Kupitia Kundi la  Uvccm Ndugu Asia Halamga Ameendelea Kutimua Vumbi Katika Kutafuta Kura za Chama Cha Mapinduzi Ndani Ya Jimbo La Hanang.

Ambapo aliendelea kupita kata kwa kata Mtaa kwa Mtaa ,Kijiji kwa Kijiji ,soko kwa Soko na mwisho  Kumalizia Mkutano Wa Kumnadi Diwani Wa Kata ya Ganana ,Mgombea Ubunge Jimbo la Hanang Eng Samwel Hhayuma Pamoja Na Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Dr John Pombe Magufuli.

Aidha Ndugu Asia Halamga AmewKumbusha Wana Hanang ya Kuwa  Waichagua  CCM kwasababu imeleta Nidhamu Serikalini Mfano leo ukienda Ofisi yeyote unapokelewa kama Mfalme na Kuhudumiwa kwa wakati yote hayo ni CCM.

Pia Ndugu Asia Halamga Amewaambia wananchi wa Hanang' kuwa serikali ya CCM imepunguza Gharama za uwekaji wa Umeme toka Tzs 321,000/= hadi leo hii Tzs 27,000/= Hakuna Kama CCM.

Wana Hanang Na WaTanzania Kwa Ujumla Tumchague tena Ndugu John Pombe Magufuli Kwa Makubwa Aliyoyafanya lakini tusiache kumpa Mbunge na Diwani wa CCM ili aweze kufanya kazi vizuri.

Ziara yake hyo pia ilihudhuriwa na Mwenyikiti wa vijana Mkoa Ndugu Moses Komba na Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Ndugu Stanley.

#Magufuli5Tena.
#KaziIendelee.

No comments:

Post a comment