Friday, 21 August 2020

VIDEO YA MISS BUZA YAVUNJA REKODI KATIKA MUZIKI WA SINGELI


Video ya wimbo wa Rayvanny alioshirikiana na Dulla Makabila ‘Miss Buza' imevunja rekodi na kuwa video ya kwanza ya muziki wa Singeli kutazamwa na watanzaji wengi zaidi katika mtandao wa YouTube ikiwa na watazamaji (views) Milioni 5.6 hadi kufikia sasa.

Miss Busa imewekwa katika mtandao wa YouTube, March 26, 2020, katika Channel ya Rayvanny.

Wanga Wabaya, Meja Kunt akiwa na Lava Lava inakuwa video ya pili ya muziki wa singeli kuwa na watazamaji (views) wengi, ikiwa na watazamaji Milioni 4. video hiyo iliwekwa kwenye Channel ya LavaLav, February 13, 2020.

Huku video ya Hujanikomoa ya Harmonize inakuwa video ya tatu ya muziki wa Singeli kuwa na watazamaji (views)  wengi, ikiwa na watazamaji Milioni 2.3 mpaka kufikia sasa.

Video ya wimbo huo, Hujanikomoa uliwekwa February 08, 2020 yani ni siku tano kabla ya kuwekwa wimbo wa Wanga Wabaya wa Meja Kunta na Lava Lava.

No comments:

Post a Comment