Saturday, 1 August 2020

MKURUGENZI ILALA AWATAKA WANANCHI KUJIFUNZA KILIMO BANDA LA ILALA


NA HERI SHAABAN,MOROGORO

MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala  Jumanne Shauri amewataka wananchi kutembelea banda la Halmashauri ya Ilala kujifunza kilimo.


Mkurugenzi Shauri aliyasema hayo leo ,katika banda la Ilala wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wakulima Kanda Mashariki Mkoani Morogoro.

Alisema manispaa ya Ilala imejipanga vizuri kwenye maonyesho ya mwaka huu katika banda la Ilala kuna kilimo cha kisasa.

"Katika banda letu la Ilala  kuna kilimo cha Kisasa, kilimo cha mjini,umwagiliaji kwa kutumia mfumo wa matone, kilimo cha mboga bila kutumia udongo, usindikaji wa mazao kwa kuongeza thamani na kiimo cha mbogamboga kwa kutumia Kitalu " alisema Shauri.


Shauri alisema katika banda la  halmashauri ya Ilala kuna vitu vingi vya kujifunza katika sekta ya Kilimo  na mifugo

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Manispaa ya Ilala Estther     
Masomhe  alisema pia katika banda La Ilala kuna uzalishaji na utunzaji mazao ya jamii nafaka mbogamboga ,matumizi ya dhana bora za kilimo.

Masomhe alisema  kilimo kikingine kinachopatikana katika banda la Ilala kilimo cha uyoga, kilimo cha uwiano,mbinu za kudhibiti wadudu waharibifu wa mimea.


Pia alisema uchakataji ngozi, uzalishaji wa bidhaa za ngozi wa kutumia teknorojia rais, uhimilishaji mifugo, uzalishaji na utunzaji marisho,uchakataji maziwa, ufugaji bora wa mifugo.

Aidha mkuu wa Idara Kilimo Esther alisema kwa upande wa uvuvi banda la Manispaa hiyo kuna uchakataji samaki ,utotoleshaji vifaranga vya samaki, ufugaji samaki katika Mabwawa, utengezaji wa chakula cha samaki na ufugaji chakula katika matanki.


Mwisho
Agosti Mosi
Nane nane Morogoro

No comments:

Post a comment