Monday, 17 August 2020

AZAM FC YAMSAJILI MSHAMBULIAJI HATARI KUTOKA ZIMBABWE.


Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube, kutoka Highlanders FC ya nchini humo.

Dube ambaye ni mmoja ya washambuliaji hatari Zimbabwe, akiwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo cha wachezaji wa ndani, anakuja Azam FC kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.

Benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, limeridhishwa kwa kiasi kikubwa na uwezo wake kwa muda wote waliomfuatilia hadi kuamua kumsajili.

Huo unakuwa usajili wa saba kwenye kikosi cha Azam FC, katika dirisha hili la usajili kwa ajili ya msimu ujao, wengine wakiwa ni kipa David Kissu, beki wa kushoto Emmanuel Charles.

Wachezaji wengine walioongezwa ni kiungo mkabaji, Ally Niyonzima, viungo washambuliaji, Awesu Awesu, Ismail Aziz na Ayoub Lyanga.

No comments:

Post a Comment