Na Allawi Kaboyo Bukoba.
Vyumba vya madarasa 1297 vinahitajika kwenye shule za msingi kwa Halmashauri  Ya wilaya  Bukoba mkoani kagera ili kufikia mahitaji ya vyumba vya madarasa 2334 ili kuwezesha wanafunzi katika halmashauri hiyo kuweza kupata elimu yao kwa hali iliyo salama na nadhifu.
Hayo yamesemwa  na afisa elimu msingi Devotha Mwesigwa wakati wa hafla ya kupokea nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Karama na vyumba vya madarasa viwili shule ya msingi Ruzila zilizoko kata Rukoma wilayami humo julai 27,mwaka huu  vilivyo jengwa na  shirika la World visioni kanda ya Kagera.
Alieleza kuwa halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu 2107 na vyumba vya madarasa 1297 hali inayofanya kuwa changamoto kwa walimu na wanafunzi  sule za msingi wanaoishi katika mazingira hayo.
“Halmashauri ya wilaya Bukoba inajumla ya nyumba za walimu 227 ikiwa uhitaji ni nyumba 2334 madarasa yaliyopo 1197 ikiwa shule za msingi za serikali ni 141 na walimu jumla yao ni 1138  na wanafunzi ni 830000 halmashauri nzima na tangu kuanza kwa kwa utaratibu wa elimu bila malipo halmashauri imepokea kiasi cha Zaidi ya shilingi bilioni 3.5 hadi sasa” Alieleza Mwalimu Devotha.
Alisema kuwa mazingira bora ndiyo humfanya Mwanafunzi kusoma vizuri na kufikia malengo ya kupata taaluma inayotakiwa na serikali inafanya ushirikiano na mashirika yanayosaidia kwemye miundombinu mbalimbali.
Aliongeza kuwa, Serikali imekuwa ikielekeza nguvu katika elimu Zaidi kuwapatia wananchi elimu itakayosaidia kujiongoza kwa mambo mbalimbali ya upanuaji wa uchumi na taifa kuwa na wananchi wenye elimu ambapo ameongeza kuwa tangu kuanza kwa elimu bila malipo wastani wa wanafunzi umeongezeka kutoka.
 Magembe Petro  ni mratibu wa shirika la world vision  alisema, ujenzi wa miundombinu hiyo ulifanywa baada ya kutembelea shule hizo na kuangalia uhitaji ulikuwa ukikabili shule hizo, ambapo alisema katika shule ya Ruzila ambayo awali kabla ya kujenga vyumba viwili vya madarasa wanafunzi walikuwa wakisomea kwenye miundombinu mibovu.
“awali wakati tunakuja na mfadhili hapa kulikuwa na wanafunzi wanasomea kwenye chumba kilijengwa na fito na matope haikuweza kuridhisha ndipo tukapanga kujenga vyumba viwili leo julai 27 tunavikabidhi kwa halmshauri husika”alisema Petro
 Aidha alisemna kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo ulighalimu shilingi milioni 125 ambapo nyumba ya mwalimu iligarimu shilingi milioni 69.5 ikiwa  vyumba vya madarasa  viligalimu milioni 56 ambayo ni garama ya vifaa vya jamii na viwanda.
Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya msingi Karama Leina Malichades alisema, ujio wa miundombinu hiyo itasaidia kutotembea umbali mrefu wa Zaidi ya  kilomita 14 kutoka katika makazi ya kuishi ya sasa kufata eneo la kazi.
“Hii nyumba itasaidia changamoto za kutembea  urefu mkubwa kufuata shule tunaomba serikali na mashirika kuendelea kujitoa kwa moyo kutupatia nyumba nyingine”alisema Malichades
Alisema  matumizi ya garama ya maisha yaliongezeka kwani kila kukicha hutumia usafiri wa bodaboda  na kulipia kodi ya nyumba .
Share To:

Post A Comment: