Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu amewaonya wafanyabiashara wanaohujumu miundombinu kama sehemu ya malighafi ya viwanda kuacha mara moja tabia hiyo, vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.

Waziri Zungu ametoa onyo hilo wakati alipotembelea kiwanda cha Nondo cha Hong yu Steels (T) Co. Ltd kilichopo Kibaha mkoani Pwani ambacho kimesimamisha uzalishaji kutokana na ukosefu wa malighafi.

Kwa upande wake Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Mashariki Bw. Arnold Mapinduzi amesema watawachukulia hatua wafanyabiashara wa vyuma chakavu wanaokiuka utaratibu uliowekwa bila kujali rangi wala cheo cha mhusika.

Utaratibu uliowekwa na serikali unawataka wafanyabiashara wa vyuma chakavu kujaza fomu ya ukusanyaji vyuma hivyo ili kuiwezesha NEMC kufahamu wanakopata vyuma hivyo, hatua inayolenga kudhibiti hujuma inayofanyika kwenye miundombinu mbalimbali.
Share To:

Post A Comment: