Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha Ndugu Omary Lumato Akihutubia mabinti wa Shirikisho la Vyuo na Vyuo vikuu mkoani Arusha.
 Baadhi ya mabinti wa Shirikisho la Vyuo na Vyuo vikuu mkoani Arusha wakifuatilia kwa makini mada zikiendelea kutolewa ukumbini.
Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa  (MNEC) Bi. Anna Agatha Msuya akifuatilia kwa makini kongamano la mabinti wa Shirikisho waVyuo na Vyuo Vikuu mkoani Arusha.



 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Bi.Yasmin Bachu akifuatilia kwa makini kongamano la mabinti wa Shirikisho waVyuo na Vyuo Vikuu mkoani Arusha

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Arusha Ndugu Omary Lumato amewaasa mabinti wa Shirikisho wa Vyuo na Vyuo Vikuu kuhamasika na kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu tarehe 25 mwezi oktoba wakiamini wanaweza ili kutimiza kusudio lao la kuzaliwa na ndoto zao kwenye maisha.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UVCCM Omary Lumato  kwenye Kongamano la Binti chuo kikuu lililoandaliwa na shirikisho la vyuo na vyuo vikuu mkoani hapa na kusema kuwa "Nawapongeza kwa kuandaa kongamano hilo kwani ni fursa yakujenga ccm ya mika 50 ijayo yenye dira na maono mapya ya kutambua
kiongozi mwanamke".


Aliongezea kwa kusema kuwa wasihangaike na Ng’ombe bali wahangaike na ndama kwani
ccm ya mika 50 ijayo iwe ndio maono yao kwa kuanza kujitokeza kuomba nafasi za kugombea uongozi nao kama umoja utawapa nafasi kwa kuwaunga mkono kutimiza malengo ya ndoto zao.


Kwa Upande wake Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa MNEC Anna Agatha Msuya katika kongamano hilo amewasihi mabinti hao kuwa kuna mambo matano wanatakiwa kufahamu mabinti wa kitaanzania kuwa wamezaliwa wakiwa viongozi ndani ya familia hivyo kuna uongozi wa kuzaliwa na uongozi wa kujifunza na wasikatishi ndoto zao kwa maneno ya aina yoyote.

Aidha aliwataka kuangalia dira na maono yao na kutosita kujitokeza kuomba nafasi za kiuongozi kwa kujiamini kuwa wanaweza ila watambue kuwa watakutana na changamoto mbalimbali zisiwakatishe tamaa.

“Tambueni nyinyi mnaweza kubeba maono yenu msitegemee kiongozi wa kuzaliwa pekee bali mnaweza kuwa viongozi wa kujifunza kwa kubeba maono ya kulijenga taifa kwa kuangalia kusudio la uwepo wa kila binadamu hapa duniani”alisisitiza

Awali akitoa Ushuhuda katika Kongamano hilo aliyekuwa diwani wa viti maalum halmashauri ya Arusha DC Munna Talib alisema kuwa ukishakuwa mtoto wa kike tambua kuwa wewe ni kiongozi angalia maono na dira yao jitokeze na kujipanga kutimiza ndoto zako za kuwa kiongozi kwenye jamii inayokuzunguka bila uoga na kujiamini wewe ni kiongozi.

Nae Mwenyekiti wa shirikisho la vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Arusha Baraka Mungure alisema kuwa watahitaji viongozi wanawake wabeba maono nchi wenye mchango kwa taifa letu wenye wito wa kutambua umuhimu wa kiongozi mwanamke kwa kuwa mabadiliko yanaanza na wao.

Kwa Upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Yasim Bachu akitoa mada alisema
kuwa changamoto anazokutana nazo mtoto wa kike zisiwe kikwazo cha kutimiza malengo ya mpango wa mungu kufikia maono na dira ya ndoto zao za kiungozi kwa kukatishwa tama na wakongwe ndani ya siasa.

Aliwaeleza kuwa anayo imani nao kubwa wakitumia muda wao vizuri na kujitambua kuwa wanaweza kuwa viongozi hakika watakuwa kama wao na kuja kuwa mabalozi wazuri kumkombo mwanamke katika kujenga taifa lenye usawa kiuongozi kwa 50 50

Aliyekuwa Mbunge wa viti maalum kupitia kundi ya walemavu Amina Mollel amewataka vijana hao kuongeza na kujali muda wao kwa kujitokeza kuomba nafasi na kugombea kwani wao teyari ni viongozi wajao katika taifa hili wakitambua kuwa wanaweza.




Share To:

Post A Comment: