Mwanansiasa wa upinzani nchini Tazanzania Tundu Lissu hii leo ametangaza rasmi nia ya kuwania urais kupitia chama chake cha Chadema.

Akizungumza kwa njia ya mitandao akiwa ughaibuni, Lissu ametangaza nia ya kuwania urais nchini Tanzania, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2020.

Lissu ametangaza nia hiyo akiwa ughaibuni ambako alipelekwa miaka takribani miaka mitatu iliyopita baada ya kushambuliwa vibaya kwa risasi na watu wasiojulikana.

''Sasa ninapenda kuwataarifu rasmi kwamba nimetangaza rasmi nia yangu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Tayari nimeshawasilisha taarifa rasmi ya kutangaza nia hiyo kwa katibu mkuu wa chama chetu kama iliyoelekezwa kwenye maelekezo yake kwa wanachama wa chama chetu.''

Katika hotuba yake iliyopeperushwa mubashara mchana huu kwa njia ya mitandao ya kijamii, Lissu ameahidi kuwa endapo atapata ridhaa ya kuiongoza Tanzania serikali yake haitalipiza kisasi.
Share To:

Post A Comment: