NA HERI SHAABAN

HALMASHAURI ya Ilala wadhimisha siku ya mazingira Duniani kwa kupanda miti shule ya Msingi Kiwalani kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Segerea na wadau wa mazingira kutoka  Arena Recycling Industry
Environmental conservation community of Tanzania (ECCT)

Akizungumza wakati wa upandaji miti shule ya Kiwalani mgeni rasmi,,Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea Shamsudin Hemed aliwataka wananchi wa Jimbo la Segerea kutunza mazingira na pia wakikata mti wapande mti.

"Nawapongeza wadau wa mazingira katika kuadhimisha siku hii nawataka muwe  mabalozi wazuri katika kutunza kutunza mazingira katika jimbo letu la Segerea kila kaya waweke utaratibu wakupanda miti mitano katika maeneo yao "alisema  Shamsudin.


Alisema utunzaji wa mazingira ni muhimu yanatuletea hewa safi ,vyanzo vya maji,  hivyo kila mtu anatakiwa kutunza mazingira yatutunze.


Shamsudin alisema katika Jimbo la Segerea kuna kata 13 kila mwaka wameweka utaratibu wa kupanda miti shule zake zote za msingi na sekondari.

Aidha shamsudin alitaka elimu ya utunzaji mazingira itolewe kuanzia shule za msingi ili wanafunzi wafahamu umuhimu wa mazingira.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiwalani Uzeely Mwambo alisema shule hiyo imeanza mwaka 1979 imeweka utaratibu wa utunzaji mazingira pia ina mwalimu wa Mazingira kutokana na likizo ya corona wanafunzi wapo nyumbani kwa sasa wameshindwa kushiriki tukio la hili.


Naye Mwakilishi wa Afisa 
Mazingira manispaa ya Ilala Kezia  Nashon alisema siku hii ni muhimu tufuate Kauli Mbiu yetu tutunze Mazingira yatutunze.

Mwisho
Share To:

Post A Comment: