ImageMkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Sirro amesema kuwa, Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa Nchi za Ukanda wa Kusini Mwa Afrika (SARPCCO) wamekubaliana kwa pamoja kuendelea kupambana na uhalifu ili kutokutoa mwanya kwawahalifu ndani ya jumuiya hiyo.
IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati aliposhiriki mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) mkutano ambao umelenga kuwekeana mikakati mbalimbaliya kiutendaji ndani ya jumuiya hiyo.
Akizungumzia suala la uhalifu kwa njia ya mtandao IGP Sirro amesema kuwa, jambo kubwa ambalo jumuiya hiyo wamekuwa wakipambana naloni kuendelea kufanya mafunzo ya mara kwa mara hasa kwa wapelelezi ili kuwa na vifaa, uweledi na uelewa juu ya masuala ya uhalifu wa kimtandao.
Katika hatua nyingine IGP Sirro ameelezea juu ya ushirikiano kati ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.



Share To:

Post A Comment: