Na Woinde Shizza,Arusha

Uongozi wa bar maarufu ya picnic iliyopo katikati ya jiji la Arusha umeelezea mikakati mbalimbali ambayo wanaitekeleza kipindi hiki katika kupambana na janga la ugonjwa hatari wa corona.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa bar hiyo, Bodia Kaaya alisema kwamba kufuatia janga la corona wao kama watoa huduma wamechukua hatua mbalimbali kama kuhakikisha wahudumu wao wanavaa barakoa muda wote wakati wa kutoa huduma.

Kaaya,alisema kwamba mbali na barakoa pia wamehakikisha wameweka ndoo za maji na sabuni katika milango ya kuingilia ndani ya eneo lao ili kunawa mikono yao kabla hawajaingia kupata huduma.

Alisema kwamba wametoa vitakasa mikono lakini pia wanapulizia dawa katika meza mbalimbali zilizopo ndani ya eneo lao kama njia mojawapo ya kupambana na corona.

Pia alisisitiza wanafuata kanuni zote zilizotolewa na wizara ya afya nchini ambapo wanawafundisha watumishi wao namna ya kuchukua tahadhari na ugonjwa wa corona.

"Tunachukua tahadhari zote tunazoelekezwa na wizara ya afya lakini pia tunawafundisha wafanyakazi wetu namna ya kujikinga na gonjwa hili"alisema meneja huyo

Naye mtumishi wa bar hiyo,Elisante Charles alisema kwamba wao kama watumishi wameelekezwa hatua zote za kuchukua kujikinga na gonjwa la corona kama kuvaa barakoa muda wote wawapo kazini.

Charles, alisema kwamba baadhi ya watumishi wa afya wamekuwa wakipita mara kwa Mara katika bar hiyo na kuwapa elimu mbalimbali na kufanya ukaguzi na kuiomba serikali kufanya hivyo kwenye maeneo mengine

"Witumishi wa idara ya Afya hapa Arusha wametupatia semina ya kutosha namna ya kujikinga na corona wakati wa kutoa huduma pia vifaa vipo vya kutosha uongozi umezingatia hilo na kufanya kazi kuwa rahisi alisema Charles

Share To:

msumbanews

Post A Comment: