Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu (kulia) akitoa msaada wa fedha kiasi cha Sh.800,000 kwa Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali cha  Upendo, Kata ya Iglanson wilayani Ikungi mkoani Singida jana. Kutoka kushoto ni Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Kata ya Iglanson, Zubeda Abrahaman, Mwenyekiti wa UWT,  Kata ya Minyughe, Elizabeth Bakari na Mwenyekiti wa UWT,  Kata ya Iglanson, Sarah Napegwa.
Mwenyekiti wa UWT,  Kata ya Iglanson, Sarah Napegwa (kushoto), akimkabidhi fedha hizo Katibu wa UWT,  Kata ya Iglanson, Zubeda Abrahaman.


Na DottoMwaibale, Singida.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ametoa msaada wa fedha kiasi cha Sh.800,000 kwa Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali cha  Upendo, Kata ya Iglanson ili waweze kuongeza mtaji wa kununua mazao ya biashara.

Akizungumza wakati akitoa msaada huo jana, Kingu alisema anatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwasaidia wanawake hao ambao wanafanya shughuli za ujasiriamali.

"Nafanya jambo ili katika kipindi hiki kwa ajili ya kwenda na wakati wa msimu huu wa mavuno kwa sababu wanawake hao wananunua alizeti, ufuta na mahindi ambayo watakuja kuyauza kwa faida" alisema Kingu.

Alisema amekuwa akifanya hivyo kwa ajili ya kuwasaidia wanawake hao ambao kikundi chao kimesajiliwa na licha ya kupata mikopo kutoka Halmashauri yeye kama Mbunge wao ameona ni vema kuwaunga mkono kwa fedha kidogo ambazo Mungu amekuwa amembariki.

Kingu alisema anaimani fedha hizo watazizalisha na kuweza kuwasaidia katika matumizi ya familia zao na pia kujiendeleza kwenye suala zima la maisha yao.
Alisema fedha hizo hajawakopesha ili waje wamrudishie bali ametoa kama mtaji na ukikua wataendelea kukopesha katika vikundi vyao na mtaji utabaki kwenye kikundi.

Akipokea msaada huo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Kata ya Iglanson, Sara Napegwa alisema fedha hizo zimetolewa na mbunge huyo kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake wa Kikundi cha Upendo ambazo watazigawa katika vikundi vya ufugaji wa nyuki, kuku, ushonaji, ukamuaji wa mafuta ya alizeti, kilimo cha mbogamboga na matunda.
Share To:

Post A Comment: