KATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona kampuni ya Qwihaya General Enterprises Co Ltd imetoa vifaa kinga vya ugonjwa huo kwa kundi la vijana wa bajaji na Bodaboda mjini Mafinga wilaya ya Mufindi .

Mwenyekiti wa medeva wa bodaboda Obadia Kipondamali  akishukuru kwa msaada huo jana  alisema ni nadra sana wao kukumbukwa lakini kampuni hiyo ya Qwihaya ameweza kuwakumbuka.

"Tunashukuru kwa huu msaada hasa tenki kubwa la maji na vitakasa mikono vitatusaidia sana, tupo kwenye mazingira hatarishi,"* amesema Kalinga.

Meneja wa Qwihaya  Ntibwa Mjema alisema wanaendelea kugawa vifaa hivyo kupitia kampeni ya kampuni hiyo ya kusambaza vifaa vya corona ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na ugonjwa huo.


Diwani wa Kata ya Kinyanambo, Chesco Livale  alisema msaada huo ni maombi yake kwa kampuni ya Qwihaya ili kuwakinga wananchi wa eneo lake dhidi ya Corona.

Mwenyekiti wa CCM wa kata ya Kinyanambo, ameziomba kampuni nyingine za kizalendo kushiriki vita dhidi ya corona kama ilivyo Qwihaya General Enterprises Co Ltd.

Kwa upande wake, Mjema amesema baada ya wafanyakazi wake kujikinga wameamua kushirikiana na Serikali kusaidia maeneo mengine.

Kampuni ya Qwihaya tunashiriki vita dhidi ya corona kwa vitendo kwa  kutoa  vifaa ili wenzetu waendelee kujikinga," amesema.

Qwihaya ni kampuni inayomilikiwa na mzalendo Leonard Mahenda ikijihusisha na kutengeneza nguzo za umeme.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: