Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Tabata Mtamban  Biligita Nchimbi akimuonyesha Katibu wa Mbunge wa Segerea nyumba zilizoanguka Bonde la Msimbazi katika mafuriko jana

Na Heri Shaban

MVUA kubwa zaleta mafuriko katika  Bonde la Tabata Msimbazi na kudondosha nyumba 30 Mtaa wa Tabata Mtamban  Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani.

Nyumba hizo zimedondoka jana katika bonde hilo na kusababisha wakazi wa eneo hilo kukosa makazi  yao baada kaya zisizokuwa zikiishia eneo hilo kuhama.

Akizungumza katika   eneo la tukio Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Mtambani Biligita Nchimbi alisema nyumba hizo zimekwenda na mafuriko baada mto huo kuacha njia yake na kufuata makazi ya watu na kusababisha waanga kwa kukosa nyumba .

Mwenyekiti Nchimbi amefikisha kilio chake kwa serikali akiomba fedha zilizotengwa kwa ajili ya ya utekelezaji wa Bonde la Msimbazi zifanye kazi yake kwa wakati endapo serikali itachelewa hasara kubwa itatokea kwa sababu ya mto huo kukosa mwelekeo wake na kuingilia eneo la makazi.

Wananchi hawa baadhi yao walikuwa nje ya mitaa 60 kutoka eneo la Bonde lakini nao wamekumbwa na mafuriko kufuatia mafuriko hayo  kuacha kupita katika mkondo wake  "alisema Nchimbi.

Alisema katika Nyumba hizo za wananchi wake kulikuwa na watu muhimu ambao walikuwa wakiisaidia serikali katika shughuli za  kijamii pamoja na chama.

Kwa upande wake Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Segerea Bw.Shamsudin Hemed ambaye alikuja kuwapa pole wakazi wa Tabata Mtamban  kwa niaba ya Mbunge Bonah Ladslaus alisema athari zilizotokea katika bonde hilo ni kubwa kufuatia maji kuacha mkondo wake.

Bw, Shamsudin alisema amejionea athari katika bonde hilo huku watu wakiendelea kukimbia makazi yao kutokana na maji hayo kuwa na nguvu.

"Mh, Mbunge  Bonah kwa sasa yupo Bungeni Dodoma nitawasiliana naye kwa nilichokiona eneo hili aweze kuzungumza na Mamlaka husika kwa ajili ya hatua za haraka kwani mvua mwaka huu ni kubwa na zinaendelea kuleta athari katika bonde hili la Msimbazi "alisema Shamdudin.

Shamsudin aliwataka wakazi waishio Katika eneo hilo kuvuta subira wakisubiri serikali kupatia ufumbuzi tatizo hilo.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: