Na Allan Isack,ARUSHA

TUME ya Taifa ya uchaguzi nchini (NEC), imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo  maofisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Wilaya na kata,maofisa Tehama wa Wilaya,waandishi wa vituo vya kupigia kura  na BVR Operator.

Shughuli  ya utoaji wa mafunzo imefanyika kwa mikoa 12 nchini,na  itakwenda  sambamba na zoezi la uwekaji wazi wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na  uboreshaji wa  daftari la kudumu la wapiga kura awumu ya pili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo,Ofisa Elimu kutoka (NEC),Titus Mwanzalila, amesema  mafunzo hayo yatakwenda sambamba na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili kwa mikoa 12 ya Arusha, Kilimanjaro,Manyara, Tanga, Simiyu, Shinyanga, Geita,Kagera, Kigoma,Mwanza, Mara, na Tabora.

Alisema awamu ya pili mzunguko wa kwanza wa uwandikishaji wa taftari la kudumu la wapiga kura itafanyika kwa siku tatu, Aprili 17 mwaka huuu hadi Aprili 19.

Licha ya kuzungumza hayo,alisema zoezi hilo litakwenda sambamba na kuwaandikisha wapiga kura wapya waliotimiza umri wa mika 18,na wale wenye sifa lakini hawakujiandikisha awamu ya kwanza,kutoa kadi kwa waliopoteza kadi,kuhamisha taarifa kwa waliohama kata au jimbo,kurekebisha taarifa zilizokosewa na kuondoa taarifa za waliopoteza sifa.

Hata hivyo,alisema ili kupambana na maambukizi ya virusi vya corona NEC,imeandaa mfumo wa kidigitali kwa wananchi kuhakiki taarifa kwa kutumia simu na kutembelea tovuti ya tume.

Msimamiwa uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini,Dk.Maulidi Madeni,alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za uchaguzi mkuu wa nchi.

“Mafunzo haya yanatolewa kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za uchaguzi mkuu wa nchi kwamba nilazima kuwepo kwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kabla na baada ya uchaguzi ili kurobesha,kuandikisha na kuhakiki taarifa za wapiga kura,”alisema Madeni.

“Sisi kama serikali tuna wajibu wa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa mafunzo kwa watu ambao watakwenda kusimamia zoezi la uboreshaji wa daftari,”.alisema Madeni

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: