Mlipuko wa ugonjwa wa Corona nchini Marekani  unaweza kufikia kilele chake wiki hii, amesema afisa mwandamizi wa mamlaka ya afya nchini humo.

Licha ya ishara za kwanza ya kuwepo kwa utulivu katika maeneo tofauti ya nchi hiyo , viongozi kadhaa wa kisiasa wamebaini kwamba kurudi kwa shughuli za kawaida za uchumi kunategemea kuongezeka kwa vipimo kwa watu ili kusahihisha kuwa maaambukizi bado yapo.

Marekani ambayo ni nchi ya tatu yenye watu wengi zaidi ulimwenguni, imeathirika zaidi na janga hili la Covid-19, ambapo watu 22,800 wamefariki dunia kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa Jumatatu na shirika la habari la Reuters. 

Watu zaidi ya 10,000 wamefariki dunia katika Jimbo la New York pekee, na zaidi ya visa 500,000 vya maambukizi vimeripotiwa katika jimbo hilo.

Wataalamu wanasema takwimu zinazoloewa ni za chini ikilinganishwa na idadi halisi ya watu wanaokufa na ugonjwa huo majumbani siku hadi siku. 

Lakini Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa na Kinga Robert Redfield,anasema wanakaribia kufikia kilele cha maambukizi hayo.

Idadi ya vifo vilivyoripotiwa kote nchini Jumapili ilikuwa 1,513, ikiwa ni idadi ndogo zaidi ya kila siku iliyoripotiwa tangu Aprili 6.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: