Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Kwa mwaka wa fedha 2019/20 Halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi
Bilioni 765.48 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani ambapo   Katika
kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 Halmashauri zimekusanya Jumla
ya Shilingi bilioni 527.31 ambayo ni asilimia 69 ya makisio ya mwaka.

Hayo yamesemwa  jana JIJINI Dodoma  na Waziri wa nchi,Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI]Mhe.Seleman Jafo
wakati akizungumza na wanahabari wakati wa kuwasilisha taarifa  Ya
Mapato Ya Ndani Ya Halmashauri Julai, 2019 Hadi Machi, 2020 .

Waziri Jafo amesema Uchambuzi wa taarifa za mapato ya ndani ya
Halmashauri katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 umeonesha
ongezeko la mapato yaliyokusanywa kutoka Shilingi Bilioni 449.82 kwa
kipindi cha Julai, 2018 hadi Machi, 2019 na kufikia Shilingi bilioni
527.31 katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 ambalo ni
ongezeko la  Shilingi bilioni 77 sawa na asilimia 17 .


Katika kipindi hicho  Waziri Jafo amesema Halmashauri ya Jiji la Dar
es Salaam imeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya
mapato kwa asilimia 78 ya makisio yake ya mwaka huku Halmashauri ya
Jiji la Dodoma imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya
kwa asilimia 55 ya makisio yake ya mwaka

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeongoza kundi la Halmashauri za
Manispaa ambayo imekusanya asilimia 100 ya makisio yake ambapo  Katika
kundi hili Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imekuwa ya mwisho ambapo
imekusanya kwa asilimia 49 ya kwa Mwaka wa Fedha 2019/20

Kwa upande wa Halmashauri za Miji, Halmashauri ya Mji wa Njombe
imeongoza kwa kukusanya kwa asilimia 130 ya makisio ya mapato ya ndani
kwa mwaka wa fedha 2019/20 ambapo Halmashauri ya Mji wa Handeni
imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 43 ya makisio ya mapato ya
ndani kwa mwaka wa fedha 2019/20.


Aidha, kwa kundi la Halmashauri za Wilaya,  Waziri Jafo aliendelea
kufafanua kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeongoza kwa kukusanya
asilimia 126 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa Fedha 2019/20
wakati Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imekuwa ya mwisho katika
kundi hilo kwa kukusanya asilimia 30 ya makisio ya mapato ya ndani kwa
mwaka wa Fedha 2019/20.


 Mapato ya Ndani ya Halmashauri kwa Kuzingatia Aina za Halmashauri kwa
Kigezo cha Wingi wa Makusanyo ,Katika kipindi hicho Halmashauri ya
Jiji la Dodoma imeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya
Shilingi bilioni 36.04 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa ya
mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi bilioni 8.83.

Kwa upande wa Halmashauri za Manispaa   ,Manispaa ya Ilala imeongoza
kwa kukusanya Shilingi bilioni 43.14 huku  Halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma Ujiji imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya
Shilingi Bilioni 1.20.

Katika kipindi hiki, Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa wingi
wa Mapato katika Halmashauri za Miji ambapo imekusanya Shilingi 7.02.
Halmashauri ya Mji wa Mbulu imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo
imekusanya Shilingi Milioni 671.78.

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imeongoza kwa kukusanya mapato mengi
kwa Halmashauri za Wilaya ambapo imekusanya Shilingi Bilioni 5.78.
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imekuwa ya mwisho katika kundi hili
ambapo imekusanya Shilingi Milioni 343.70.

 Katika Matumizi ya Mapato ya Vyanzo vya Ndani ya Halmashauri Waziri
Jafo aliendelea kufafanua, Katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi,
2020 Halmashauri zimetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 329.53 ambayo ni
asilimia 63 ya mapato halisi yaliyokusanywa kuanzia Julai, 2019 hadi
Machi, 2020. 


Kati ya matumizi hayo, Shilingi Bilioni 186.75 zimetumika
kwenye matumizi ya kawaida na Shilingi Bilioni 142.80 zimetumika
kwenye matumizi ya maendeleo. Aidha, katika kipindi hicho kiasi cha
Shilingi Bilioni 34.83 kimetumika kwenye miradi ya maendeleo ikiwa ni
bakaa ya mapato ya ndani ya mwaka wa fedha 2018/19 ambayo ni asilimia
76.5 ya bakaa yote (Shilingi Bilioni 45.54), hivyo kufanya jumla ya
matumizi ya miradi ya maendeleo kufikia Shilingi Bilioni 169.20.

Aidha,Waziri Jafo aliainisha baadhi ya  changamoto zilizojitokeza
katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kipindi cha Julai, 2019 hadi
Machi, 2020 ni pamoja na Bado zipo baadhi ya Halmashauri hazisimamii
kikamilifu matumizi ya mashine za kukusanyia mapato (POS).

Pia  Waziri Jafo alitumia fursa ya kuainisha mikakati ya kukabiliana
na changamoto hizo kuwa ni pamoja Upangaji wa Bajeti za Mapato ya
ndani uzingatie uwezo halisi wa wa mapato ya kila chanzo (Revenue
potential) na Halmashauri zitumie takwimu sahihi katika kuandaa
Makisio ya mapato ya ndani. Pia Halmashauri ziongeze udhibiti wa
mifumo ya ukusanyaji wa mapato ili kuondoa mianya ya upotevu wa
mapato.
Share To:

Post A Comment: