Mtuhumiwa wa mauaji ya binti wa kazi Salome Zakaria ambaye Jana akishindwa kufikishwa kizimbani kutokana na Ugonjwa wa Covid 19 picha na maktaba akipandishwa mahakamani siku ya kwanza ya kutajwa kwa kesi hiyo 
Mtuhumiwa wa kesi ya Mauaji ya mfanyakazi wake wa ndani, Mkami Shirima (30) ameshindwa kuletwa mahakamani kutokana na sababu ya maambukizi ya corona.

Shirima alikuwa afikishwe leo katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Arumeru, lakini ameshindwa kupandishwa kizimbani kwa kile kilichoelezwa ni kupunguza msongamano mahakamani ili kuzuia maambukizi ya Corona .

Taarifa zilielezwa mahakamani hapo ni kwamba utaratibu wa mahakami kwa sasa ni kuzuia msongamano mahakamani kwa washtakiwa ambao mashauri yao hayajakamikika upelelezi

Kutofikishwa mahakama.

Shauri hilo lililopo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Analia Mushi lilishindwa kusomwa mbele ya mahakama hiyo badala yake karani wa mahakama ndiye aliyetoa taarifa za kuahirishwa kwa kesi mbalimbali ikiwemo kesi ya Mkami Shirima..

Mkami Shirima anashitakiwa kwa kosa la kumuua kwa kumpiga na fimbo Mfanyakazi wake wa ndani ,Salome Zacharia, Marchi 6 mwaka huu katika eneo la Ilkuirei ,Sakina nje kidogo ya jiji la Arusha na kusababisha kifo chake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 21 mwaka huu itakapokuja tena mahakamani hapo .


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: