Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Katika  kutekeleza majukumu ya Wizara ya Madini kwa  Mwaka 2020/2021,
Bunge limeridhia  na kupitisha makadirio ya Jumla ya shilingi
62,781,586,000 kwa ajili ya Matumizi ya Wizara na Taasisi zake.

Akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma April 21 ,2020   hotuba ya
Makadirio Ya Mapato na Matumizi Ya Fedha Kwa Mwaka 2020/2021 Waziri wa
Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko alisema  Mchanganuo wa Bajeti hiyo ni
kama ifuatavyo:-

 (i)Bajeti ya Maendeleo ni shilingi 8,500,000,000. ambazo zote ni
fedha za ndani; na (ii)Bajeti ya Matumizi ya Kawaida ni shilingi
54,281,586,000. ambapo shilingi 21,045,927,000. ni kwa ajili ya
Mishahara na shilingi  33,235,659,000 ni Matumizi Mengineyo (OC).

Aidha Waziri Biteko alisema katika Mwaka 2020/2021, Wizara inapanga
kukusanya jumla ya shilingi 547,735,863,597 ikilinganishwa na shilingi
476,380,613,492 kwa mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia
14.98.

Kati ya fedha zitakazokusanywa, shilingi 526,722,547,000 sawa na
asilimia 96.16 zitawasilishwa Hazina na shilingi 21,013,316,597 sawa
na asilimia

84 85 3.84 zitatumika na Taasisi zilizo chini ya Wizara.


Katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini  Waziri Biteko alisema
Wizara  itaendelea kutenga maeneo yanayofaa kwa Wachimbaji Wadogo;
kuwapa elimu kuhusu uwepo na faida za kuuza madini yao katika masoko
yaliyoanzishwa; kutoa huduma nafuu za kitaalam kwa Wachimbaji Wadogo
ikiwa ni pamoja na kuwafahamisha kuhusu uwepo wa mashapo katika maeneo
yaliyobainishwa na kutengwa kwa ajili yao; na kutoa elimu kwa
wachimbaji wadogo kuhusu utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya
madini yenye tija na namna ya kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za
fedha.

Waziri Biteko aliendelea kufafanua kuwa Kwa kipindi kinachoanzia mwezi
Julai, 2019 hadi Februari, 2020 jumla ya kilo 25,435.12 za dhahabu
zenye thamani ya shilingi 2,772,331,030,317.99 zilizalishwa na
kusafirishwa nje ya nchi kutoka katika Migodi Mikubwa na ya Kati.

Migodi hiyo ni pamoja na Geita Gold Mine, North Mara Gold Mine, Pangea
Minerals (Buzwagi Mine), Bulyanhulu Gold Mine, Shanta Mine (New
Luika), STAMIGOLD Company (Biharamulo Mine) na Busolwa Gold Mine
(Tanzania).
 Aidha, katika  kipindi hicho kilo 10,102.43 za dhahabu zenye thamani
ya Shilingi 975,430,320,903.97 zilizalishwa na wachimbaji wadogo wa
madini.

Kuhusu ujenzi wa ukuta  wa Mererani  Waziri Biteko alisema
umesababisha kuongezeka kwa makusanyo ya Serikali kwa takribani mara
13 ya kiwango kilichokuwa kikikusanywa awali ambapo katika mwaka 2019
makusanyo yaliongezeka na kufikia shilingi 2,150,000,000
ikilinganishwa na shilingi 166,094,043

zilizokusanywa mwaka 2017 kabla ya ujenzi  wa ukuta huo.


Akiwasilisha  Taarifa Ya Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Nishati Na
Madini Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu Ya Wizara Ya Madini (Fungu 100)
Kwa Mwaka Wa Fedha 2019/2020 Pamoja Na Maoni Ya Kamati Kuhusu
Makadirio Ya Mapato na Matumizi Kwa MwakaWa Fedha 2020/2021  Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Dunstan Luka
Kitandula   alisema  kwakuwa Wizara bado haijapata Fedha za maendeleo
zilizoidhinishwa na Bunge Shilingi 7,039,810,200.00 kutoka hazina
hivyo Kamati inasisitiza kuwa Serikali ihakikishe kabla ya kwisha kwa
mwaka wa Fedha 2019/2020, maombi ya Fedha ambayo yamepokelewa Hazina
yawasilishwe kwa Wizara ili Wizara  iweze kutekeleza kikamilifu
majukumu yake.

Akiwasilisha maoni ya kambi Rasmi ya Upinzani Naibu Msemaji Mkuu kambi
 Rasmi yaUpinzani  katika Wizara ya Madini  Mhe.Joseph Haule  amesema
kuna umuhimu wa kupitia upya muundo wa Wizara ya Madini na kufanya
marekebisho katika idara ama taasisi zenye Majukumu yanayofanana ili
kuondoa gharama zisizohitajika .
Pia Kambi hiyo ya Upinzani imeishauri Serikali kuwaambia Watanzania
hatima ya majadiliano ya ACACIA  na fedha ambazo ilitakiwa kulipwa
kama zilishalipwa  kwa sababu ni jambo la umma watanzania
walishirikishwa tangu Mwanzo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: