Wednesday, 11 March 2020

UHAKIKI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI KUANZA MACHI 17,2020,MSAJILI ASEMA HAKUNA CHAMA KITAKACHOFUTWA
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe Jaji Mstaafu, Francis Mutungi akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020 kwa lengo la kuimarisha uhai wa vyama hivyo.Pichani juu kulia ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza na kushoto ni  Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ally Ahmed
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza akiwasilisha mada kuhusu mambo yanayotakiwa kuzingatiwa na Vyama vya Siasa wakati wa Zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa katika mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa(RPP), Mhe. Jaji Mstaafu, Francis Mutungi na viongozi wakuu wa Vyama vya Siasa nchini leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihusu kuwapitisha viongozi hao katika hatua zitakazopitiwa wakati zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa. Linalotarajiwa kuanza tarehe 17, Machi 2020.
Wajumbe wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini wakifuatilia mada wakati wa wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji Mstaafu, Francis Mutungi (hayupo pichani) na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020 kwa lengo la kuimarisha uhai wa vyama hivyo.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa mkutano huo.


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF akichangia mada wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji Mstaafu, Francis Mutungi (hayupo pichani) na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020 kwa lengo la kuimarisha uhai wa vyama hivyo.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo ya CHADEMA,Benson Kigaila akiomba ufafanuzi wa jambo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji Mstaafu, Francis Mutungi wakati wa mkutano huo.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini uliofanyika leo jijini Dar

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Juma Abdulla Juma Saadala akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji Mstaafu, Francis Mutungi (hayupo pichani) na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020 kwa lengo la kuimarisha uhai wa vyama hivyo.

Majadiliano ya Mkutano huo yalipokuwa yakiendelea.

Picha na Michuzi JR-Michuzi Media.


====== = ======   ========  ========


MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi amesema zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa linalotarajia kuanza tarehe 17 Machi mwaka huu,halina malengo ya kufuta usajili wa vyama hivyo na badala yake ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019.

Jaji Mutungi aliyasema hayo leo Jumanne (Machi 10, 2020), wakati wa Mkutano wake na Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchiniuliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Bunge Jijini Dar es Salaam.

Jaji Mutungi alisema malengo ya zoezi hilo litakoendeshwa na Ofisi yake ni kuona namna bora ya kujenga uelewa wa pamoaj wa sheria ya vyama hivyo katika kipindihiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Alisema kuwa ni wajibu wa vyama vyote vya siasa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kuwa Serikali haiwezi kuahirisha zoezi hilo na badala yake kuvitaka vyama hivyo iwapo vina hoja ya msingi ni vyema zikawasilisha katika Baraza la Vyama hivyo ili kuweza kupatiwa mwafaka wa pamoja wa makubaliano.

Kwa mujibu wa Jaji Mutungi alisema katika muda uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu, kwa mujibu wa sheria Ofisi yake haiwezi kufuta usajili wa chama chochote cha siasa na hivyo kuwataka Viongozi wa vyama vya siasa kuondoa dhana potofu kuwa Serikali imepanga kufuta baadhi ya vyama vyenye usajili wa kudumu nchini kutoka katika daftari la Msajili wa Vyama vya siasa.

Aliongeza kuwa zoezi la uhakiki linaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kuwa zoezi hilo si geni kwa kuwa serikali imekuwa ikiendesha zoezi la uhakiki wa taasisi, makampuni na mashirika mbalimbali na hivyo kwa vyama vya siasa zoezi hilo halina utofauti wowote kama ilivyo kwa taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Jaji Mutungi alisema hakuna sababu ya vyama hivyo kujenga hofu kuhusu zoezi hilo kwani limekusudia kubaini changamoto mbalimbali zinazovikabili vyama vya siasa nchini ili kuweza kutoa mapendekezo kwa Serikali na hivyo kuimarisha mshikamano uliopo ili kukukuza na kuimarisha demokrasia nchini.

‘’Tumeamua kukutana na wadau ili kuondoa ombwe kuhusu utekelezaji wa sheria ya Vyama vya siasa ya mwaka 2019, kwani suala la uhakiki lipo kisheria, serikaliinatambua changamoto zilizopo katika vyama vya siasa na zoezi hili limekusudia kujenga msingi wa pamoja wa kujitathimini wapi tulipotoka, tulipo na tunapokwenda’’ alisema Jaji Mutungi.

Akifafanua zaidi Jaji Mutungi aliwataka Viongozi wa vyama vya siasa kulitazama zoezi hilo katika taswira chanya kwa kuwa zoezi hilo limekusudia kujenga amani ndani ya vyama hivyo katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini kote mwezi Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba alisema vyama vya siasa havina pingamizi kuhusu zoezi la uhakiki na badala yake aliitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa muda wa miezi mitatu ili kuhakikisha kuwa vyama vyote vinakamilisha masuala mbalimbali ya kiutendaji na taratibu zote za 

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vyote vinapaswa kuwa na wanachama wenye uwezo wa kiutendaji ikiwemo kuwa na kadi za uanachama, hivyo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa havina budi kuongeza muda ili kutoa nafasi kwa vyama hivyo kuweza kuhakiki wanachama wake.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda aliitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutengeneza mwongozo wa mfumo wa adili za uongozi ndani ya vyama vya siasa na utaratibu huo uendeshwe katika vikao vya Baraza la Vyama vya siasa nchini.

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Viongozi wa vyama vya siasa nchini, Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo aliipongeza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa utaratibu wa kufanya vikao kwani utaratibu huo haukuwepo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini miaka 28 iliyopita.

No comments:

Post a comment