Na John Walter-Manyara
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kanda ya kaskazini imewakutanisha watu wenye mahitaji muhimu katika wilaya ya Babati na kuwapatia semina maalum kuhusu usajili wa namba za simu kwa alama za vidole na huduma nyingine za mawasliano.

Akifungua semina hiyo Mjini Babati Leo Machi 14,2020, Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu, ametoa wito kwa jamii kulitilia uzito swala hilo la kusajili laini,na kwamba  ambao hawajapata kitambulisho cha Taifa (NIDA), Mamlaka husika itawasaidia kupata namba zao,sambamba na wale ambao hawajajiandikisha NIDA wapo tayari kwa ajili ya kuwasaidia ili wajiandikishe wapate kitambuluisho cha hicho muhimu.

Kitundu amesema jambo walilolifanya TCRA kuwakumbuka wenye mahitaji maalum ni la kupongezwa kwa kuwa Mawasiliano ni haki ya kila mmoja.

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum ameeleza kuwa Lengo la semina hiyo ni kutoa elimu kwa watu wenye mahitaji maalum, kuhusu zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya mfumo wa alama za vidole ,pia kuangalia changamoto mbalimbali walizonazo katika huduma za Mawasiliano.

Mhandisi Imelda, amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaendelea kuhakikisha inadhibiti vitendo vyote vya uhalifu wa kimtandao vinavyofanywa na watu wasio waaminifu.

Katibu wa shirikisho la watu wenye ulemavu mkoani Manyara Peter Sanka, amesema wanaishukuru TCRA kwa kuwathamini na kuwapatia semina hiyo.
Ameshauri kuwepo na mfumo utakaowawezesha wasiosikia na wasioona kuweza kuwasiliana na ndugu,jamaa na marafiki zao bila usumbufu.

Naye Mwenyekiti wa watu wasioona wilaya ya Babati John Pantaleo amesema katika mawasiliano  kwao changamoto kubwa ni mtu wa kuwasomea ujumbe lazima awepo,hakuna usiri,tunaomba serikali itusaidie uwepo wa simu ,ambazo tunaweza kusoma ujumbe kwa kusikia sauti ,na iwe katika lugha ya kiswahili ambapo itaweza kuondoa utegemezi kwa kiwango kikubwa.

Makundi yaliyoyonufaika na elimu hiyo kutoka  Mamlaka hiyo ni wenye huoni hafifu, Viziwi,  walemavu wa ngozi na viungo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: