Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilala Jumanne Shauri, akizungumza katika makabidhiano ya ujenzi wa madaraja ya jimbo la Ukonga Ulongoni A,Zimbili na Ulongoni B Arnatogluo Halmashauri ya Ilala leo
Meya wa halmashauri ya manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza katika makabidhiano ya ujenzi wa madaraja ya jimbo la Ukonga Ulongoni A,Zimbili na Ulongoni B Arnatogluo Halmashauri ya Ilala leo,
Mkuu wa wilaya Ilala Dkt.Sophia 
Mjema akizungumza katika makabidhiano ya ujenzi wa madaraja ya jimbo la Ukonga Ulongoni A,Zimbili na Ulongoni B Arnatogluo Halmashauri ya Ilala leo, (kulia) Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mwita Waitara

.........................................................
NA HERI  SHAABAN
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala wamekabidhi ujenzi wa madaraja matatu  Jimbo la Ukonga kwa wakandarasi.

Madaraja hayo yaliokabidhia jimboni  humo  daraja la Zimbili, Ulongoni A na Ulongoni B ambapo kazi za ujenzi zinatarajia kuanza Aprili Mosi mwaka huu.

Utekelezaji wa mradi huo wa unafanywa na DMDP sambamba na ujenzi wa barabara za kiwango cha lami.

Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala Jumanne Shauri alisema leo  manispaa hiyo inatekeleza miradi ya DMDP kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia ujenzi utakaoghalimu shilingi za Kitanzania bilioni  115.

" moja ya miradi inayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa  madaraja makubwa mawili ambayo ni daraja la ulongoni B litakalo jengwa pamoja na Barabara kiwango cha lami Kilomita 7.5 na daraja la Zimbili Ulongoni A"alisema Shauri.

Mkurugenzi Shauri alisema ujenzi wa daraja la Ulongoni B na barabara kilomita 7.5 kitajengwa na stendi ya Kinyelezi ya kisasa na Mkandarasi M/s China Railway Seventh Gruop kwa gharama za shilingi 17,608,000,955.08.

Aidha Shauri alisema daraja la Zimbili Ulongoni  A litajengwa na Mkandarasi wa M/s Chongqing Internationl Construction Corporation kwa gharama za  shilingi  4,304,066,255.20  ujenzi wake utakamilika ndani ya miezi kumi tangu kuanza kwa ujenzi wake madaraja yote yapo mto Msimbazi.

Huku Mkuu wa Wilaya Ilala Dkt. Sophia Mjema alisema amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi aliyepewa tenda ya ujenzi mpaka ujenzi utakapoisha endapo zikitokea changamoto  katika ujenzi huo watoe taarifa Mamlaka husika kwa kufuata utaratibu.

"Awali eneo hilo la Ulongoni A na Ulongoni B kulikuwa na changamoto kubwa kutokana na kukosekana kwa mawasiliano kwa juhudi za Rais wetu John Magufuli sasa serikali yetu pendwa ya awamu ya tano fedha zimepatikana sasa ujenzi wake unaanza rasmi naomba wananchi tuunge mkono juhudi za Rais " alisema Dkt.Mjema.

 Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mwita Waitara Mbunge wa Ukonga (CCM) aliwataka Wananchi waache malumbano katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali badala yake waache Wakandarasi watimize wajibu wao.

Waitara alitaka mikataba ya masharti ya ujenzi  yazingatiwe waache wakandarasi watimize wajibu wao ili kuteleza miradi kwa wakati.

Meya wa halmashauri ya manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto alipongeza serikali na kuwataka wakandarasi  kumaliza ujenzi ili wananchi wa Jimbo la Ukonga wanaotumia vivuko hivyo kuwaondolea adha inayokuwa wakipata kila wakati wa mvua kwa kukosa mawasiliano.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: