Tuesday, 18 February 2020

Zitto Kabwe Akutwa Na Kesi Ya Kujibu

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT – Wazalendo) Zitto Kabwe amekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka matatu ya uchochezi yanayomkabili katika Mahakama ya Kisutu.

Zitto amepewa siku nne kuanzia tarehe 17 Machi-20 Machi 2020 kuwasilisha ushahidi wake wa utetezi. 

Hivyo, Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Machi 17, 18, 19 na 20, 2020

Katika kesi ya msingi, Zitto anabiliwa na mashtaka matatu yote ya uchochezi, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28 mwaka 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

No comments:

Post a comment