Saturday, 8 February 2020

Waziri Kigwangala Azindua Bodi Mpya ya Tanapa


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dr.,Hamis Kigwangala amezindua bodi mpya ya Tanapa iliyoongezewa muda wake na Raisi John Pombe Magufuli  baada ya kumaliza miaka 3 ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia Tanapa na kuhakikisha utalii endelevu kwa maslahi mapana ya taifa.

Kigwangala ameipongeza wajumbe wa Bodi hiyo kwa kuteuliwa na kuaminiwa na Raisi Magufuli katika kusimamia bodi hiyo  ambayo imepewa jukumu  la kusimimia Tanapa kwa kipindi kingine cha miaka 3 baada ya kufanya vizuri.

Ameitaka bodi hiyo kuja na mikakati ya kuongeza idadi ya watalii wa nje na watalii wa ndani  pamoja na kuhakikisha utalii wa endelevu  na shirikishi kwa jamii zinazozunguka hifadhi.

Aidha ameitaka bodi hiyo kutatua migogoro baina ya hifadhi na wananchi ili kuhakikisha kunakua na utalii endelevu ambao ni matunda ya ushirikishwaji wa jamii zinazozunguka hifadhi

Pia ameagiza  bodi hiyo kuhakikisha zoezi la uwekaji wa mipaka katika hifadhi unafanyika ili kulinda maeneo ya hifadhi yasivamiwe  na kuathiri shughuli za uhifadhi.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali Mstaafu George Waitara amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu bodi hiyo ilifanikiwa kuanzisha jeshi usu,kupambana na ujangili pamoja na kusimamia uhifadhi endelevu kwa maslahi ya taifa.

Kamishna wa Uhifadhi Tanapa ,Dr.Allan Kijazi amesema kuwa wataendelea kushirikiana na bodi hiyo katika kuimarisha na kuendeleza utendaji kazi bora wa Tanapa na hifadhi zilizoko chini yake pamoja na kuongeza mapato yanayotokana na utalii.

No comments:

Post a comment