Na Woinde Shizza, Arusha 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya wazazi Taifa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk Edmond Mndolwa amesema mradi wa nyuki ulioanzishwa na jumuiya hiyo unatakiwa kuanzishwa pia na jumuiya nyingine za chama hicho.


Akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wilaya ya longido jana  Dkt Mndolwa alisema mradi wa nyuki ni kitega uchumi ambacho kinaingiza fedha nyingi kwa muda mfupi hivyo ni vyema jumuiya nyingine zikaanzisha mradi huo ikiwemo UVCCM na UWT.

Alisema mradi huu wa Nyuki utasaidia kuongeza ajira katika nchi yetu na utasaidia kuwaondoa vijana wengi vijiweni kwani wataweza kujiajiri wenyewe ,aidha alibainisha kutoka na hilo ataenda kuishauri kamati ya chama chake kuingiza mradi huu Wa Nyuki katika ilani ya uchaguzi ili uwe mradi Wa Taifa.


"Mradi wa nyuki ni mradi wenye tija na nitahakikisha unaongia kwenye rasimu yetu ya ilani ili uwe sehemu ya miradi itakayotekelezwa na serikali mahususi kwa ajili ya kutoa ajira kwa vijana hawana ajira ili waweze kujiajiri kupitia mradi huo".

Alisema  kwa sasa soko la asali ni kubwa sana duniani na pia bei ni kubwa tofauti na zao lingine  lolote lile  kwani  kwa sasa Lita moja ya asali inafika shilingi elfu 12000wakati bidhaa zingine kama mchele ni shilingi 2500,sukari ni shilingi 2600 na hiyo inaonyesha tu kuwa asali ni zao ambalo linaela kuliko mazao mengine yoyote Yale.

Aidha katika ziara hiyo ya utekelezaji Wa Wa ilani , aliweza kukabidhi
Mashine ya kufetulia matofali yenye thamani ya shilingi milioni sita na lakimoja ,viti vya plastiki 100 vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu  pamoja na mizinga ya Nyuki  100 yenye thamani ya shilingi milioni 20 vitu vyote hivi vikiwa vimetolewa na Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha Hezron mbise.

Alimpongeza Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha kwa kutoa bidhaa hizo ambapo aliwataka viongozi wengine waige mfano wake huku akiwaonya wagombea ambao ni wanachama Wa chama cha mapinduzi wanaoenda kugombea nafasi mbalimbali wasithubutu kuhonga ilo wapate nafasi.

"Napenda kuwaomba wagombea Wa nafasi za ubunge na udiwani ,kutohonga wananchi fedha badala yake ,wahonge chama cha mapinduzi  kwa kuwaletea maendeleo ,huku akibainisha iwapo atabainika mtu alieonga binadamu  hatachukuliwa hatua ikiwemo kukatwa jina lake" alisema Mndolwa.


Kwa upande wake Mwenyekiti Wa chama cha mapinduzi wilaya ya Longido Josefu Sadala alishukuru jumuiya hiyo kwa kuwapa miradi hiyo nakuhaidi kuwa wataitunza na kuisimamia vyema ,uku akibainisha  kuwa vitu hivi vitasaidia kuwapa ajira vijana Wa wilaya  hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: