Mkuu wa dawati la jinsia la polisi Kigoma Inspeta Doris alisoma taarifa yake kwa balozi wa umoja wa ulaya alipotembelea katika ofisi hizo Mkoani Kigoma
Editha Karlo,Kigoma
WANANCHI wa Mkoa wa Kigoma wamekuwa na mwamko wa kutoa taarifa kwa wakati kwenye madawati ya jinsia  ya polisi juu ya matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia na watoto  yanayowatokea.

Akisoma taarifa kwa  kwa balozi wa umoja wa ulaya Manfredo Fanti,Mkuu wa dawati la jinsia  ofisi za Kigoma mjini Inspeta Doris alisema kuwa kutokana na elimu ambayo wameitoa kuhusu ukatili wa jinsia na watoto pamoja na umuhimu wa kutoa taarifa  kwa wakati mara wanaposhuhudia tukio likitokea  imepelekea wananchi kutoa taarifa ya matukio mengi  katika vituo vya madawati ya jinsia vilivyopo katika Wilaya zote.

"Sasa hivi jamii imeacha kuona aibu kutoa taarifa pindi wanapokumbana na matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto badala yake imekuwa na mwitikio mkubwa wa kutoa taarifa ya matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto wanayofanyiwa"alisema

Alisema kutoka kipindi cha January 2019 hadi kufikia january 2020 jumla ya matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia na watoto yaliyotolewa taarifa ni matukio 63 kwa mwaka 2019/201, ambapo mwaka 2019 kulikuwa na matukio 40 na 2020 matukio 23.

Inspeta Doris alisema kuwa askari wa dawati la ukatili wa  jinsia na watoto wamekuwa wakifanya  juhudi mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kiutoa elimu mashuleni na vijijini hali iliyopelekea wananchi kuona umuhimu wa kutoa taarifa vituoni vya ukatili wa kijinsia na watoto.

"Tunaweza kuona mwaka huu matukio yameongezeka kwasababu wananchi wameshapata elimu ya kutosha na hivyo kuona umuhimu wa kutoa taarifa kwenye vituo'alisema

Alisema kupitia ofisi za dawati wameweza kutoa huduma na kushughulikia kesi mbalimbali zinazohusu matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto kwa mwaka 2014 kesi nyingi walipata mafanikio mahakamani.

Alitaja changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na mashahidi wanageuka kesi inapofika mahakamani kwa mwaka jana wamepata kesi saba ambazo mashahidi waligeuka mahakamani.

Alisema wamejipanga kutoa elimu kuanzia ngazi ya familia,mashuleni,mikutano ya hadhara kwa kushirikiana na vingozi wa dini na wadau wengine kama wasaidizi kisheria,kividea,ustawi wa jamii,kiwode na mtakuwa.

Balozi wa nchi za umoja wa ulaya Manfredo Fanti alilipongeza dawati kwa kazi nzuri wanayofanya ya kusaidia jamii na kwamba wapo tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ambavyo vimekuwa vikishusha utu wao.

Hayo ameyasema leo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi  baada ya kukagua kutembelea na kukagua ofisi ya dawati la jinsia la polisi Mkoani Kigoma iliyojengwa kwa ufadhili kupitia mradi wa kigoma pamoja(KJP).

Pia ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa ushirikiano wanaotoa na kusema kuwa wataendelea kuwa marafiki wa serikali ya Tanzania ,pia amewataka wanaume nao wajitokezs kwenye madawati ya kijinsia yaliyopo katika Wilaya zao ili kupata ushauri na suluhu pindi wanapotendewa vitendo vya kikatili toka kwa wanawake.

Naye Scolastica julias Mkurugenzi wa miradi Legal services facility alisema ni jukumu la wazazi kufuatilia watoto kujua wanafanya nini na wapo wapi kukaa nao na kuongea nao.

''Kutokana na maisha tunayoishi unakuta kwenye chumba kimoja unawalaza watoto kwa kuwachanganya watoto wa kike na wakiume wote wanalala kwenye chumba kimoja kama wazazi inabidi tubadilike yale mambo ya zamani watoto wanaelewa na jamii sasa hivi hayopo"alisema

Alisema kwa wao wasaidizi wa kisheria ambao wanahakikisha watu wanapata haki wao wamejipanga kuhakikisha wanatoa elimu,kuhusu haki ya mtoto,haki ya uzazi na elimu yoyote inayoendana na maswala ya sheria.

''watu wanakosa uelewa na elimu ndo maana kesi zikifika mahakamani wanakataa,kwa mfano mimba za utotoni mtu anaambiwa usinitaje nitakupa cherehani anafikiria maisha yake ndo yamefikia hapo ila huyo akieleweshwa kwamba anatakiwa kusoma baadae aweze kusaidia familia yake unakuta anaweza kufanya vizuri na kuja kusaidia familia baadae"alisema
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: