Na Ahmed Mahmoud Arusha


Ongezeko la idadi  ya  wanafunzi wanaokatishwa  masomo  kwa kupewa  mimba limeibua hofu kwa  wadau  wa  maendeleo wa  ndani  na  nje  ya  nchi,Ambao  baadhi  yao   wameshindwa  kuvumilia na kuamua  kuungana  na  serikali kusaidia  kukabiliana  na tatizo  hilo
La Mimba kwa wanafunzi wakike.

 Na Miongoni wa  wadau  hao kutoka nje ya nchi ni pamoja na  wahisani Kutoka Nchi ya Korea  ambao   wamejitolea  kusaidia nakwa  Upande  wa  wadau wa  ndani ni pamoja na  Taasisi ya Kifedha ya Benk  ya  Exim  ambayo  imetoa  milioni  25 kwa  ajili  kutengeneza  vitanda ikiwa  ni mchango  wao kusaidia kuwawezesha  wanafunzi kulala shuleni

Akipokea misaada hiyo Mkuu wa  mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo amewashukuru wahisni hao kwa hatua  hiyo  kubwa huku akiwataka wengine kuiga  mfano huo ambao umeongeza  nguvu katika jitihada za  serikali za kutekeleza mkakati wake  wa  kuimarisha upatikanaji wa  mabweni mashuleni ambao ni sehemu ya suluhisho la  tatizo la mimba kwa  wanafunzi hasa   wanaotembea umbali mrefu kwenda na kurudi ambao  wamekuwa  wakikabliliwa  na  changamoto nyingi njiani.

Kwa upande  wa Mkurugenzi wa  Taasisi hiyo ya Kifedha ya  Exim kutoka makao makuu Dar es salam Bw Jafari  Matundu  amesema msaada  waliotoa  ni sehemu ya kuchangia sekta ya Elimu  na  wataendelea  kushirikiana  na wadau  wengine  kusaidia  miradi  ya maendeleo  ya wananchi

Uku shirika la Maendeleo la Korea Koika nalo  limetoa  wataalam  10 wa  kujitolea  kuwaelimisha  wanafunzi  wa  shule  za msingi  na Sekondari     juu ya Masomo ya Tehama na sayansi  kuwasaidia  katika Maisha na masomo  yao  ambayo  yameanzia  kwenye  shue  ya sekondari  ya Mrisho  Gambo iliyoko  Kata  ya Olasiti .

Hata hivyo  viongozi  wa mkoa  wa  Arusha  wamepokea  mashine  moja  ya kisasa  ya kutolea  nakala iliyotolewa  na baadhi  ya wadau  yenye thamani  ya milioni  11 ambayo  inatarajiwa  kusaidia kufanikisha mkakati  wa  mkoa  wa Arusha  wa  kuandaa  Mitihani  ya  majaribio  kwa wanafunzi  inayofanywa  na shule  zote za mkoa wa Arusha .

Pamoja  na  mkoa  wa Arusha  kuwa  miongoni  mwa mikoa  kumi bora katika  ufaulu kitaifa bado  unakabiliwa  na tatizo  kubwa  la  wanafunzi  kukatishwa  masomo  kwa ajili ya mimba sababu zinazotajwa  wengi  wao  kusoma  shule  zakutwa ambazo  hulazimika kutembea  umbali mrefu  kwenda  shule.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: