Monday, 17 February 2020

VIONGOZI WA UPINZANI ACHENI KUICHAFUA NCHI KIMATAIFA RUDI NYUMBANI TUZUNGUMZEMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris amewataka Viongozi wa Vyama vya Upinzani nchini wanaozunguka ughaibuni Nchi mbalimbali wakiiachafua Nchi na Rais Magufuli warudi Nyumbani kwa ajili ya Majadiliano

Ameyasema Hayo wakati wa  Hafla ya kuwapokea na kuwakabidhi Kadi rasmi madiwani wawili na wanachama Kadhaa wa Upinzani walioamua kurudi CCM wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu CCM Taifa Dr Bashiru Ally akiwa Morogoro Vijijini hafla imefanyika Ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro Mtaa wa Saba Saba na kuhudhuriwa na wanachama, wakereketwa na Viongozi Mbalimbali

Mwenyekiti Innocent amesema"Ujumbe Wangu kwa Viongozi wa Upinzani wanaozunguka Kusema Nje ya nchi warudi Nyumbani kama Kuna Jambo la kuzungumza waje Tuzungumze kuendelea Kusema Nje Nini Maana yake? Tumekosa fedha za benki ya Dunia Kisa Mtu amesema bila kutambua athari zake ni pamoja ni kwa ndugu Jamaa, Wazee Hata watoto wake"pia amesisitiza umuhimu wa Kurudi nyumbani na Kusemea kwenye Nafasi zao Maana Wengi ni wabunge kuliko kusemea Nje na Kuonekana wasaliti.

"Kama Kuna mambo wanahisi yanahitaji kuzungumzwa warudi waje Ndani Tuzungumze na Bahati Nzuri wengine ni wabunge na Wengine walikuwa wabunge wana Forum Bungeni ya Kuzungumza. Ila wakikimbilia Nje ni kielelezo tosha wanaichafua Nchi kwa maslahi yao sio kujenga Nchi"

Pia Mwenyekiti Kalogeris Amegusia Siri ya mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro ambapo wamepongezwa na Katibu Mkuu CCM Taifa Dr Bashiru Ally kwa kuwa wabunifu kudumisha Amani na Mshikamano "Siri ya Mafanikio Mkoa wa Morogoro kwa Chama na Serikali ni Kujitambua kila Mtu Anajua nafasi yake kila Mtu anaheshimu Nafasi ya mwenzake na tunaamini Serikali ni ya Chama Cha Mapinduzi kwa Hiyo tunakaa Nayo Karibu ili Chama tuisimamie serikali yake"

Pamoja na hayo Mwenyekiti Kalogeris amewataka wanachama wa Chama hicho kuwapokea wanachama wapya na kuvunja Makundi na mtengano kama walivyoaswa na Katibu Mkuu CCM Taifa kwamba Hakuna mmiliki wa Chama hicho wote ni warithi
"Wana CCM Tuendelee kuwa wa moja tuwapende Hawa madiwani waliorudi Katibu Mkuu CCM Taifa Dr Bashiru Ally amesema Tayari kwamba wana CCM wote ni sawa Hakuna Mwenye Hatimiliki na Chama hiki"
Hafla hiyo iliongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka, Katibu Itikadi na Uenezi Mkoa Antony Mhando, Makatibu wa Jumuiya za Chama hicho, wajumbe mbalimbali na wakereketwa wa Chama hicho.

No comments:

Post a comment