Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Arusha Day wakiwa wamekusanyika tayari kwa kuwasikiliza Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za Mawasiliano Tanzania TCRA.CCC walipotembelea shuleni hapo kuwapa Elimu.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Arusha Day wakifuatilia kwa makini kile kinachoelezwa na Baraza la Ushauri wa Huduma za Mawasiliano Tanzania TCRA .CCC

Afisa Uhamasishaji kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania(TCRA.CCC)Hillary Tesha. 







Mary Shao Katibu wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA.CCC)akizungumza na ana wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha Day
Jan Kaaya Mhandisi Msaidizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha Day.
Wakwanza kushoto ni Mhandisi mwandamizi TCRA kanda ya Kaskazini akiwa na baadhi ya wajumbe wa bodi Baraza la ushauri lawatumiaji wa huduma za Mawasiliano Tanzania(TCRA.CCC 
Happyness Kaaya mmoja wa mjumbe wa Baraza la ushauri lawatumiaji wa huduma za Mawasiliano Tanzania(TCRA.CCC )ambae pia ni mwalimu katika shule ya sekondari ya Arusha Day
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Arusha Day wakiwa wamekusanyika tayari kwa kuwasikiliza Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za Mawasiliano Tanzania TCRA .CCC walipotembelea shuleni hapo kuwapa Elimu.


Na.Vero Ignatus,Arusha.
 Baraza la ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano   Tanzania(TCRA.CCC )limetoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Arusha Day kuhusiana na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii,huduma za Mawasiliano,pamoja na kuchukua maoni kutoka kwa watumiaji wa huduma hizo.

Akizungumza Afisa Uhamasishaji kutoka TCRA.CCC Hillary Tesha amesema kuwa vijana ndiyo wahanga wakubwa wa mitandao ya kijamii na wakiachwa bila kupewa elimu taifa litaishia kuwa na kizazi ambacho hakiheshimu haki za binadamu,pia watakuwa wanatumia njia hizo za mawasiliano kwa njia mbazo hazina msaada katika Maisha yao na litakuwa kama janga kwa upande wao.

‘’Tumefanya leo katika shule ya sekondari ya Arusha Day,tunampango wa kuelekea tena shulre ya sekondari ya Kikwe na chou cha Ualimu cha Patandi’’Alisema Tesha

Hadi sasa TCRA-CCC limeshatoa elimu katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza Lindi Mtwara Arusha lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa matumizi sahihi ya za mitandao zinawafukia vijana wengi zaidi ili kuweze kuokoa vijana katika matumizi ambayo siyo sahihi ya mitandao ya kijamii.

Katika mkoa wa Arusha waliweza kukutana na kikundi cha waklemavu wameweza kushauriana nao na kuchukua maoni na mambo mbalimbali wanayoweza kuyatumia katika kuboresha huduma za mawasiliano katika mkoa na Nchini kwa ujumla

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Tanzania Mary Shao aliwataka wanafunzi hao kutumia mitandao ya kijamii kwaajili ya manufaa yao wenyewe kama vile kujisomea na kujiimarisha kielimu Zaidi

‘’Wazazi wenu pamoja na walimu wenu wanajisikia vibaya sana kutokana na matendo nmayoyafanya huko mitaani kwenu,tulieni someni kwa bidii ili muweze kuja kuwa na Maisha bora hapo baadae yasiyokuwa ya aibu’’Alisema Mary

Amewataka kufahamu  kwamba zipo sharia zinazosimamia huduma hizo hivyo wasipokuwa makini wanaweza wakajiingiza kwenye matatizo yatakayoleta aibu katika Maisha yao

Amewasisitiza kuepuka kuweka picha za hovyo (nusu uchi)kwenye mitandao ya kijamii ni kujidhalilisha na kuondoa utu wao,hivyo basi mtumiaji wa huduma yeyote ana wajibu wa kutumia huduma kwa kufuata sharia za nchi

''Nani ajuae kwamba huko baadae  wanaweza kuja kuwa viongozi na taarifa zao zote zikawa wazi  bila kificho,usikubali kujilaumu baadae’’Alisema Mary

Mwisho

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: