Wednesday, 19 February 2020

TAWA WAITAKA GREEN MILES KUONDOA VIFAA VYAKE KATIKA KITALU CHA LAKE NATRON

 Mwandishi wetu,Longido
Mamlaka ya usimamizi wanyamapori nchini(TAWA) imetaka Kampuni ya Green Miles iliyoondolewa katika kitalu cha uwindaji cha Lake Natron (East),kuondoa vifaa vyake.

Kampuni hiyo iliondolewa na Serikali tangu, January 22 lakini hadi Jana watendaji wa Kampuni hiyo walikuwa hawajajitokeza  kuondoa vifaa vyao kwenye kambi inayolindwa na Askari wa TAWA,polisi na askari mgambo .

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangalla  Agost 7 mwaka jana alitangaza uamuzi wa Serikali kuiondoa Kampuni hiyo Katika kitalu hicho kutokana na kukiuka taratibu za uwindaji ikiwepo migogoro na vijiji.

Hata hivyo, Kampuni hiyo iliomba kuongeza muda hadi Desemba 16 ili kukabidhi kitalu hicho kutokana na wakati uamuzi unatangazwa walikuwa na wageni.
 Afisa wa kikosi cha kupambana na ujangili(KDU) wa TAWA Emmanuel Pius alisema  wanaitaka Kampuni hiyo kuondoa vifaa kwani ndio maamuzi ya Serikali.

"Tangu tuwaondowe Kwa nguvu hapa hawajafika kuondoa vifaa vyao hivyo tunawatakia kufika"alisema 

Hata hivyo alisema wafanyakazi walikuwa wamekamatwa Kwa kupuuza maagizo ya Serikali kuondoka Katika Kitalu hicho waliachiwa Kwa dhamana.
 Hata hivyo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Awadhi Abdalah amekuwa akipinga kuhusika na mgogoro na vijiji 23 vinavyozunguka Kitalu hicho amba vyo vimekuwa vikidai malimbikizo ya kodi milioni 329.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Gilai Lumbwa zilizopo kambi za mwekezaji huyo, Richard Mollel alisema Kwa muda mrefu wana mahusiano mabaya na mwekezaji ikiwepo migogoro ya kushindwa kuwalipa tuzo za vijiji 23.

Kampuni ya Green Miles yatakiwa kuondoa vifaa vyake Kitalu cha Lake Natron.

No comments:

Post a comment