Friday, 21 February 2020

Rais achangiwa milioni ya kuchukuwa fomuJumuiya ya wazazi mkoani Arusha Leo imemkabidhi  imemkabidhi Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi Taifa ,ambaye pia ni mjumbe Wa kamati kuu shilingi milioni moja kwa ajili ya kumchukulia fomu ya kugombea  nafasi ya Urais kwa awamu ya pili.

 Akiongea wakati akimkabidhi Mwenyekiti huyo fedha hizo Katibu mwenezi Wa wilaya ya Arumeru ambaye pia ni mjumbe Wa kamati ya utekelezaji Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha Joshua Ongura alisema kuwa kutokana na tamko LA Mwenyekiti Wa jumuiya hiyo Taifa alilolitoa December 2019 katika kongamano lililofanyika jijini Dar es salam wameona watoe fedha hizo 

Alisema kuwa katika kongamano hill jumuiya ya wazazi iliahidi kumchukulia fomu ya kugombea urais kwa awamu ya pili Mwenyekiti Wa chama hicho ambaye pia ni Rais Wa serikali ya awamu ya tano.

Alisema kwakua mkoa Wa Arusha unaanzia na alama A wameamua kuwa Wa kwanza kumchangia rais ,pia wameona watoe kwakua raid ameweza kutekeleza vyema ilani ya chama ,na kutatua matatizo ya wananchi

Akiongea Mara baada ya kuipokea Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi Taifa Ambaye pia ni mjumbe Wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi  Edmond Mndolwa aliwashukuru jumuiya hiyo kwa moyo walionyesha Wa kutoa fedha kwa ajili ya kumchukulia Rais fomu ya kugombea katika kipindi kingine

Alisema  aluhaidi Rais kumchukulia fomu ya kugombea katika kipindi kingine ,ambapo alisema iwapo mikoa yote itatoa fedha hizo itapatikana shilingi milioni selasini na moja 31 ambayo katika hizo watachikuwa shilingi milioni moja ya kumchukulia fomu Rais naingine itakayobaki ndio wataifanyia kampeni

Alizitaka  mikoa mingine kuiga na kuanza kumchangia fedha ya fomu Rais kama vile mkoa Wa Arusha ulivyofanya na ulivyoanza kutoa fedha hizo mapema.

Picha ikionyesha Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha Hezron Mbise  Kulia akimkabidhi Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi taifa ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi Edmund Mndolwa fedha zilizochangwa na jumuiya hiyo mkoa Wa Arusha kwa ajili ya kumchukulia  fomu ya kugombea nafasi ya urahisi John Magufuli  kwa kipindi cha awamu yapili ambapo jumuiya hiyo imetoa kiasi cha shilingi milioni moja  wakati alivyokuwa akihitimisha ziara yake ya Siku tano ya kukagua miradi iliotekelezwa chini ya ilani ya chama cha mapinduzi katika wilaya ya zote tano za mkoa Wa Arusha (picha na Woinde Shizza, Arusha.

No comments:

Post a comment