Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mwanaharakati huru Cyprian Musiba kwa kutuhuma za kusambaza habari  za kutaka kuuliwa  bila kuripoti   kwenye vyombo  vya dola jambo ambalo ni kinyume na Sheria.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Feb.24.2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Musiba kupitia baadhi ya magazeti hapa nchini amechapisha kulalamika kutishiwa kuuliwa na baadhi ya wanasiasa .
Hivyo Kamanda Muroto ametoa Rai  kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa habari za makosa ya jinai kwenye vyombo vya habari bila kujulisha vyombo vya dola na jeshi hilo linamshikilia Musiba kwa Mahojiano zaidi dhidi ya Malalamiko yake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: