Thursday, 13 February 2020

MBUNGE MSIGWA ASEMA SERIKALI YA CCM IRINGA IMEAMUA KUTESA RAIA WANYONGE

Mbunge wa Iringa mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mchingaji Peter Msigwa amepinga vikali hatua ya serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) kutesa raia wake .

Msigwa alisema kitendo cha  serikali ya Iringa kuwapangia bajaji barabara mbovu si tu wanawatesa bajaji bali wanawatesa raia wengine wakiwemo wajawazito wanaotumia usafiri wa bajaji .

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kukamata madereva bajaji waliofika ofisini kwake kulalamikia ubovu wa barabara ya kuelekea Kihesa .

Alisema kuwa kilichofanywa na jeshi la polisi ni uonevu na kuwa  vijana hao walifika Kwake kutoa kero kwa Mbunge wao hivyo kukamatwa kwao si sahihi kilichofanywa ni kuonesha jinsi serikali ya CCM inavyotumia jeshi hilo la polisi vibaya kunyanyasa wanyonge .

"Nimesikitishwa sana na uonevu wa jeshi la polisi dhidi ya vijana hawa wanyonge suala hili nitalifikisha bungeni na nitaendelea kuwa mtetezi wa wanyonge "alisema Msigwa

Kuwa barabara walizopangiwa madereva bajaji si vinawatesa madereva bajaji bali zinawatesa raia wote wa Iringa wakiwemo wajawazito ambao wanatumia usafiri huo kwenda Hospitali .

Hivyo alisema ataendelea kupigia kelele suala hilo kwani linakwenda kinyume na maelekezo ya Rais Dkt John Magufuli la kutaka wanyonge wasinyanyasike .

Mbunge Msigwa alilitaka jeshi la polisi kuwapeleka mahakamani vijana wote wa bajaji wanaoshikiliwa kwa  kosa la kulalamika ubovu wa barabara na makosa mengine na kama hawatafikishwa mahakamani ataweka mawakili wa kuwapigania haki yao .

Kuhusu ubovu wa barabara ya kuelekea Kihesa inayotumiwa na bajaji alisema baada ya kulalamika bajaji kwake aliamua kujitolea kutaka kununua mafuta ya kujaza kwenye Greda la Manispaa ila kabla ya kununua mafuta hayo Tarura jioni saa 12 walipeleka Greda kwa ajili ya kuanza kazi ya kutengeneza barabara ili wasimpe umaarufu .

Lakini tujiulize Siku zote walikuwa wapi kupeleka Greda hadi bajaji walalamike kwa Mbunge ndipo watoe Greda tena jioni  kweli wana hangaika sana CCM  ila nimewashika pabaya mimi nitaendelea kutetea wanyonge .

"CCM inataka kuwageuza watu mtaji wa kisiasa kuwasaidia kero zao hawataki hivi kwa akili za kawaida bajaji unazipangia barabara mbovu si kutaka kuziua bajaji CCM iwe na huruma na wanyonge hawa "

No comments:

Post a comment