Mbunge wa Dodoma Antony Mavunde kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi na viongozi mbali mbali leo 

Shule za msingi za serikali na binafsi jijini Dodoma leo zimenufaika  na ugwawaji wa Vishkwambi 700 ambavyo vitawafanya wanafunzi wa Jiji la Dodoma kusoma na kujifunza ki-eletroniki.

Hatua hiyo imekuja  kufuatia utekekezaji wa mradi wa ugawaji wa vishkwambi kupitia Shirika la PROFUTURO pamoja na DON BOSCO.

Waziri mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda ambae aliwakilishwa na mkuu wa Wilaya ya Dodoma  Patrobas Katambi alimpongeza Mbunge wa Dodoma Anthony Mavunde kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutatua changamoto za elimu,na kuzitaka shule wanufaika wa vishkwambi hivyo wavitunze na kuvitumia kuchochea ufaulu kwa wanafunzi.

"Tangu nimekuja Dodoma kama mkuu wa Wilaya,nimejifunza jambo kubwa kupitia wewe la kuwapenda wananchi wako sana na kuweka msisitizo mkubwa kwenye elimu kama silaha ya kuwakomboa wanafunzi katika Jimbo lako hngera sana  Mavunde kwa kuendelea kuboresha sekta ya Elimu ukishirikiana na wadau kama hawa PROFUTURO"

Alisema Dodoma Jiji lazima iwe tofauti na majiji mengine kiteknolojia na  hayo ni majibu kwa vitendo.

Awali akimkaribisha mgeni Rasmi,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini  Anthony Mavunde alilishukuru shirika la PROFUTURO kwa kuchangia maendeleo kwenye sekta ya elimu jimboni Dodoma kuunga juhudi mkakati wa kuigeuza Dodoma Jiji kama moja ya maeneo yenye matumizi makubwa ya Sayansi na Teknolojia ambapo wanafunzi watajifunza masomo yao ya kawaida ya kwenye mtaala ki-eletroniki.

Akitoa maelezo ya mradi mwakilishi wa Shirika la PROFUTURO na Don Bosco Net Padri Peter Mutechura alielezea namna ambavyo Shirika hilo limejikita kutoa huduma katika kuboresha sekta ya elimu kupitia Teknolojia na kuahidi kuendelea kushirikiana na Mbunge Mavunde kutatua changamoto mbalimbali za elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: