Saturday, 15 February 2020

ILALA WAZINDUA ZOEZI LA UANDIKISHAJI DAFTARI LA MPIGA KURA


NA HERI SHAABAN
HALMASHAURI ya Ilala imetenga jumla ya vituo 399 vya uwandikishaji katika daftari la mpiga kura.

Zoezi hilo limezinduliwa Wilayani Ilala jana likihushisha kata zote 36 za halmashauri hiyo na Mitaa yake 159.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri alisema zoezi hilo la uwandikishaji mwisho February 20  Mwaka huu hivyo amewataka wananchi wa Ilala waliotimiza miaka 18 watumie fursa hiyo wajiandikishe ili waweze kupiga kura.


"Serikali imetenga  siku saba kwa ajili ya kuwandikisha katika Daftari la mpiga kura  nawaomba wananchi wa manispaa yangu ambao wametimiza miaka 18 na wale ambao hawana vitamburisho wajiandikishe kukwepa usumbufu siku za mwisho "alisema Shauri.


Mkurugenzi Shauri amesema katika kata zile kubwa wameweka vituo viwili hadi vitatu ili kuwarahishisha wananchi waweze kujiandikisha.

Alisema kila mwananchi anayo haki ya kupiga kura ni Demokrasia lakini kwanza lazima ajiandikishe katika Mtaa wake.


Aidha alisema wale ambao wanatarajia kutimiza miaka 18 octoba mwaka huu  wametakiwa kujiandikisha ili waweze kupiga kura mwananchi ambaye atakosa kitamburisho hicho awezi kupiga kura.

Amewataka wananchi wa Ilala ambao wamepoteza vitambusho vyao kutumia fursa hiyo ya kujiandikisha ili waweze kupiga kura waje kuchagua viongozi bora ambao watakuja kuwaongoza na kuleta maendeleo katika kukuza uchumi wa Tanzania ya Viwanda katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano John Magufuli.

Alisema nchi yetu ifikapo Octoba Mwaka huu inatarajia kufanyika uchaguzi Mkuu wa kuchagua Wabunge, Madiwani na Rais .

No comments:

Post a comment