Sunday, 2 February 2020

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO


 
NA ANDREW CHALE, MWANZA.


Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando yenye jumla ya vitanda 950,ikitoa huduma kwa eneo la wakazi takribani milioni 18 wa Kanda ya Ziwa na Magharibi.

Inaelezwa takribani wagonjwa wapatao 300,000 hupata huduma Bugando kila mwaka, kwa wastani watoto 3800 huzaliwa kila mwaka na upasuaji mkubwa wa fani tofauti za ubingwa na ubingwa bobezi hufanyika kwa wagonjwa 11,000 kila mwaka.

Pamoja na utoaji wa tiba za kibingwa na ubingwa bobezi, hospitali hii pia hutoa ushauri kwenye maswala ya tiba, na pia ni hospitali ya kufundishia fani mbali mbali za tiba katika ngazi tofauti kwa Chuo Kikuu Katoriki cha Afya na Tiba.

Akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo  Dkt. Bahati Wajanga amesema kuwa katika kipindi cha Miaka minne wameanzisha huduma za matibabu kwa Magonjwa mbalimbali ikiwemo  Kifafa, Degedege, Magonjwa ya mfumo wa Chakula na Kifua ,Usafishaji Damu, Kansa ,Huduma za macho pamoja huduma za Meno na zingine nyingi.

Dkt. Wajanga amesema katika miaka hivi karibuni walikuwa hawana baadhi ya huduma hizo lakini sasa wanatoa hali ambayo wagonjwa wengi walikuwa wanapata Rufaa kwenda katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Amesema Huduma ambazo wameanzisha katika hospitali hiyo ni kutokana na kuwa idadi kubwa ya wagonjwa lakini kwa sasa wametatua tatizo hilo.
Magonjwa ambayo yalikuwa changamoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Ziwa Bugando ni  Macho, Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Kifua, Magonjwa Kinywa cha Meno pamoja na Kifaa na Degedege.

Amesema Serikali inatarajia kuweka mtambo wa MRI ambapo Jengo lake  limeshakamilika  kwa ajili ya kufunga kwa hivi karibuni.

Dkt. Wajanga amesema kwa mafanikio walioyapata bado kama Hospitali inaebdelea kuwekeza huduma mbalimbali za katika hospitali hiyo  katika kuokoa maisha ya Wananchi kwa utoaji wa matibabu bora ya kuokoa vifo.

"Tumejipanga kutoa huduma bora za Afya katika Hospitali yetu ya Bugando kutokana na serikali kuwekeza sekta ya Afya hivyo kazi yetu ni kutibu kuokoa maisha ya wananchi wetu" amesema Dkt. Wajanga.

Hata hivyo amesema kuwa katika miaka minne wazalisha Maji aina 17 ikiwemo na Maji tiba kwa ajili ya wagonjwa wanaotakiwa kuongezewa maji.

"Upanuzi wa Kiwanda cha kuzalisha Maji-Tiba
Hospitali imefanikiwa  kupanua kiwanda hiki ili kutoa huduma bora, na kuzalisha dawa na maji tiba ya aina 17 tofauti.

Kwasasa idara hii inazalisha wastani wa chupa 400 kwa siku , zinazoweza kukidhi asilimia 60% kwa mahitaji ya hospitali.

Kiwanda hiki kimeleta faida kadhaa kwa wananchi:
Kinazalisha aina ya dawa ambazo haziwezi kupatikana sokoni
Kinazalisha dawa kwa bei nafuu, hivyo kupunguza gharama kwa watumiaji wa mwisho (wagonjwa)" anasema.

Dkt. Majanga anasema pia wameweza kwa na Mtambo wa kfua hewa ya Oxijeni

"Mtambo huu umesaidia utoaji wa huduma bora kwa wogonjwa wanaohitaji huduma hii. Uwepo wa huduma hii umepunguza matumizi ya pesa za ndani kwa hospitali kwenda kununulia hewa hii ya oxjeni.

"Kwa wastani hospitali hutumia mitungi 20 -30 kwa siku na mtungi mmoja kwa bei ya soko Tsh. 45,000/= . Kwa sasa hospitali inaweza kuzalisha mitungi 2100 kwa mwezi, na gharama za uzalishaji ni nusu ya bei ya soko kwa mtungi.

"Uwepo wa mitambo hii ya uzalishaji oxijeni imesaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwa hospitali, na kiwango cha fedha zinazo okolewa na hospitali kwa uwepo wa mitambo hii, zimetumika kuboresha miundo mbinu kwa wananchi wanaopata huduma Bugando"

Kuhusu upanuzi na Uboreshwaji wa kitengo cha kusafisha Figo.

"Kutokana na wagonjwa wenye shida ya  figo kuongezeka ,hospitali Kwasasa ina mashine 23  kwa ajili ya wagonjwa wenye shida za figo. Uwepo wa mashine za kutosha umesaidia kupunguza muda wa kusubiri huduma hii kwa wananchi wenye uhitaji

" Uimarishwaji wa Uchunguzi wa magonjwa ya MFUMO WA Chakula/Tumbo”
kitengo pekee na kikubwa kilichopo kanda ya ziwa na magharibi  chenye vifaa vya kisasa vya kuchunguza na kutibu magonjwa mbalimbali ya mfumo wa njia ya chakula, kama vidonda vya tumbo, uvujaji wa damu kwenye njia ya chakula.


"Mashine ya Uchunguzi ya MRI kutoka Wizara ya Afya
Hospitali ya Bugando inategemea kupokea mashine ya MRI kutoka wizara ya Afya, Mashine itakayosaidia kubaini matatizo ya wagonjwa vema, kwani ugonjwa unapogundulika mapema katika hatua za awali tiba huanzishwa mapema na hivyo kupunguza madhara au vifo kwa wagonjwa, hivyo uwepo wa mashine hii, ambayo itakuwa ya kwanza kwa kanda ya ziwa na Magharibi utapunguza adha kwa wagonjwa ya kufuata huduma hizi mbali.

"Huduma  za Upasuaji wa macho zilizoboreshwa kutoka kwa Madaktari bingwa
Hospitali ya Bugando ilipokea LASER mashine, mashine kwa ajili  ya matibabu ya macho  kutoka Wizara ya Afya, Kwasasa idara hii ya macho imeimarika zaidi, kwani inamadaktari bingwa wanne, ambao wameweza kuhudumia wagonjwa wengi nakupunguza adha kwa wananchi waliokua wanalazimika kufuata huduma hizi nje ya kanda ya Ziwa.

"Takribani wagonjwa 12,000 wa macho wameonwa kwa mwaka 2019,wenye matatizo ya pressure ya macho, kisukari na waliohitaji miwani yakusomea, ambapo mpaka mwezi oktoba 2019 imefanya upasuaji kwa wagonjwa (900).

" Huduma za kibingwa za matatizo ya kinywa na  meno
Kwasasa hospitali ya Bugando inatoa matibabu ya kibingwa na ya kisasa  kwa wananchi wenye  matatizo ya kinywa na meno kutoka kwa madaktari bingwa kwa kutumia mashine za kisasa kabisa.

"Huduma za Saratani
Bugando imekuwa hospitali ya pili baada ya Ocean Road, kutoa huduma kamili za saratani (mionzi ya ndani, nje na dawa) baada ya usimikaji wa mitambo ya kisasa ya kutolea huduma.

"Hivyo imesaidia wananchi wa kanda ya ziwa na Magharibi kupata huduma bora sehemu wanayoishi na kwa haraka”

Kupitia wizara ya afya kiasi cha shilingi bilioni 5.5 kilitolewa na serikali kwaajili ya kujenga jengo la saratani na pia  kwakushirikiana na wafadhili wa serikali ya india hospitali imeweza kununua mashine nne za mionzi ( Mashine  mbili za kupangia na kutoa matibabu ya Mionzi ya nje  bilioni 3.1  na Mashine  mbili za kupangia nakutoa matibabu mionzi ya ndani milioni 700).

"Upanuzi na Ujenzi wa Vyumba vya Upasuaji vya Kisasa
Ujenzi huu, umefanya hospitali kuwa na vyumba 13 vya kisasa vya upasuaji kutoka 5 vya awali. Hivyo kupunguza muda wa kusubiri upasuaji kwa wagonjwa na kutoa matibabu ya kibingwa kupitia mitambo ya kisasa.


"Uanzishwaji wa Kliniki kwa Wagonjwa wa BIMA na Mikataba Huduma hizi zilizinduliwa na, Mh. Rais Dkt.John Joseph Pombe Magufuli tarehe 15 Julai 2019.

Huduma hizi hutolewa kwenye jengo liitwalo “Bima Building”, ambalo lina huduma zote kwa mgonjwa kuanzia kufungua faili, huduma za vipimo mbalimbali  (vya maabara na Moyo) na hatimaye kumuona daktari na kupata dawa ndani ya jengo hilo “ One stop Centre”.

Dkt. Wajanga anaeleza kuwq, aina hii ya utoaji huduma, imevutia wagonjwa, na takribani wagonjwa 300-350 hupata huduma hapa kwa siku za kazi

" Huduma maalum ya Group Therapy
Idara ya Tiba viungo imefankiwa kutoa huduma maalum “Tiba Kikundi”( tiba kwa njia ya kikundi) kwa watoto wenye mahitaji maalum mfano; mtindio wa ubongo. Huduma hii imekua msaada na rafiki kwa wazazi wa watoto hao na jamii kwa ujumla"Uboreshaji wa Huduma za Dharura. Kanda ya Ziwa
Hospitali imefanya ukarabati na upanuzi wa idara ya dharura na majeruhi, kwa sasa ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 100 kwa mpigo, kutoka idadi ya wagonjwa 50 wa awali.

MWISHO.

No comments:

Post a comment